2014-02-27 14:08:37

Mamillioni ya fedha kutolewa kusaidia ujasiliamali vijijini- Afrika Magharibi.


Rais wa Kituo cha ushirikiano katika elimu na Maendeleo endelevu CCED ,Bwana Heather Spidell na Makamu wa Rais wa IFAD, Bwana Michalel Mordasini, Jumatano walitia sahihi katika hati ya makubaliano kwa ajili ya msaada wa fedha zitakazo tolewa na IFAD, kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za utafutaji wa nafasi za Kazi kwa vijana vijijini, Afrika Magharibi na Kati , wakianza na Benin, Cameroon, Gambia na Nigeria .

IFAD , imetoa fedha hizo kwa kuona mbali , athari za baadaye iwapo vijana wa sasa watakosa ajira, hasa katika maeneo ya vijijini na kwa ajili ya maendeleo yao. Taarifa ya IFAD inaeleza, mgogoro wa kiuchumi wa dunia, umetoa vishindo vitatu katika maeneo yanayo husiana na maendeleo endelevu na kuathiri vijana duniani kote,kwamba, ukosefu wa ajira, biashara na fedha za mitaji.

Na kwamba vijana ambao ni karibia ni asilimia 70 ya wakazi barani Afrika wanakabiliwa na kishindo hiki kwa nguvu.Mbele ya uso wao kuna changamoto mbalimbali hasa jinsi ya kuweza kupata kazi nzuri yenye hadhi na kujipataia fedha na kutengeneza biashara. Vijana wengi wana mawazo mazuri katika ubunifu ambao unawapa uwezekano wa kuwapatia ajira katika maendeleo ya biashara, lakini mtaji wa kuanzia unakuwa kikwako kikubwa katika juhudi zao

Hivyo lengo la IFAD, ni kuwa na mradi kilimo endelevu, biashara na kupandikiza moyo wa ujasiria mali kwa vijana. Pia ni kuongeza ari ya kujifunza na upatikanaji wa huduma za nyongeza katika maendeleo ya biashara. Mradi unawalenga , Wanawake vijana vijijini na wanaume , wenye umri wa miaka 15-35 , ambao ni washiriki wazuri katika uzalishaji ama kilimo au shughuli zinazohusiana na masoko ya vijijini . Mrado huu utaunda vikundi vikundi kwa ajili ya kurahisisha utoaji wa msaada wa kifedha na utalaam.

Kwa ajili ajiri ya mradi huu, kwa muda wa siku tatu, tangu Februari 26-hadi 28 , inaandaliwa warsha katika Makao makuu ya IFAD Roma, kwa kwa ajili ya mapitio ya mwisho ya kukamilisha mpango wa utekelezaji na shughuli muhimu zinazohusiana na msaada huu , ikiwa ni pamoja kuzingatia ushauri wa watalaam katika kutoa vipaumbele katika uwekezaji. Pia itakuwa nafasi kwa IFAD kujifunza na kubadilishana uzoefu zaidi juu ya shughuli za vijana vijijini.









All the contents on this site are copyrighted ©.