2014-02-27 15:11:03

Haki miliki za Khalifa wa Mtakatifu Petro


Taarifa ya Vatican inasema kuhusiana na maandishi yanayotolewa na Baba Mtakatifu Francisko, mintarafu sheria za Mchungaji Mwema namba 191, inasema kwamba, kitengo cha Uchapaji cha Vatican, LEV, ndicho chenya dhamana ya kulinda na kuhifadhi haki miliki zote za Khalifa wa Mtakatifu.

Taarifa hii ilikwishawahi kuchapishwa kwenye Gazeti linalomilikiwa na Vatican la L'Osservatore Romano, toleo la tarehe 27-28 Novemba 1978. Baba Mtakatifu kunako tarehe 23 Machi 2013 amerudia kuonesha kwamba, haki zote msingi zinabaki na zitaendelea kubaki kuwa ni mali ya Kitengo cha Uchapaji cha Vatican.







All the contents on this site are copyrighted ©.