2014-02-26 14:08:15

Wito kwa ajili ya kuombea amani na utulivu nchini Venezuela


Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Katekesi yake, Jumatano tarehe 26 Februari 2014 anasema, anafuatilia kwa masikitiko makubwa yale yanayotendeka nchini Venezuela.

Anatoa wito kwa pande zote zinazohusika kuacha matumizi ya nguvu na uhasama na kuanza mara moja kujikita katika mchakato wa upatanisho na msamaha wa kitaifa unaofumbatwa katika majadiliano ya ukweli, kuheshimiana na haki kwa ajili ya mafao ya wengi.

Hizi ni juhudi zinazopaswa kufanywa kwanza kabisa na wanasiasa pamoja na taasisi zinazohusika. Baba Mtakatifu anapenda kuwahakikisha wote walioguswa na majanga haya uwepo wake wa karibu kwa njia ya sala. Anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema kuinua sala zao kwa maombezi ya Bikira Maria kwa ajili ya kuombea amani na utulivu nchini Venezuela.







All the contents on this site are copyrighted ©.