2014-02-25 12:45:54

Wimbi la wahamiaji toka Afrika laitisha Hispania


Wahamiaji zaidi ya 300 wa Morocco , hivi karibuni walivamia uzio, wakijaribu kuvuka mpaka kati ya Morocco na Hispania mkoani Melilla, maafisa wameripoti.
Katika harakati hizo, vikosi vya usalama vya Morocco , vilipambana na wahamiaji hao na kusababisha watu 27 kujeruhiwa,na wengine tisini na sita wahamiaji walikamatwa, wakati wengine 100 waliweza kuvuka mpaka. Wahamiaji wengi toka Afrika Kaskazini , hupenda kuutumia mpaka huo ulio jangwani kuingia barani Ulaya kwa lengo la kutafuta kazi na kuboresha maisha yao. Wengi wa hamajia hao ni tokea Eritrea na Somalia.

Idara ya Mambo ya Ndani ya Hispania, imethibitisha uwepo wa kasheshe hilo la wahamiaji , Ijumaa iliyopit, ambako polisi walilazimika kutumia risasi za mpira kuwazuia wahamaji kuingia Hispania. Idara hiyo imekanusha risasi hizo kusababisha wahamiaji wengine kuzama maji.








All the contents on this site are copyrighted ©.