2014-02-25 12:28:23

Uganda yapitisha sheria ya kuzuia ushoga hadharani


Serikali ya Uganda imepitisha sheria ya kuzuia vitendo na ndoa za ushoga hadharani . Sheria hiyo imeanza kazi baada ya Rais Yoweri Museveni , kuweka sahihi yake katika hati ya muswada wa sheria dhidi ya tabia za ushoga hadharani , uliopitishwa na Bunge.
Kwa kuweka sahihi hiyo, wa hivyo amekataa kunyenyekea mashinikizo yaliyo kuwa yakitolewa na viongozi wengine kama Rais Barack Obama na Mstaafu Askofu mkuu Desmond Tutu.

Kituo cha Habari cha serikali ya Uganda katika ukurasa wake wa Tweet, Jumatatu, ulithibitisha Rais Museveni kutia sahihi muswada huo akiwa Ikulu , Entebbe , na hivyo kupiga marufuku uendelezaji wa maisha mashoga nchini Uganda na wale watakao fanya kinyume , watatiwa mbaroni na kukabiliana na sheria na wanaweza kupata kifungo cha maisha jela.

Katika upekuzi wa watalaam , inasemekana wengi huingia katika tabia hii mbovu kutokana na malezi na pia wengine huwa mashoga kwa kishwawishi cha kujiajiri au kuajiriwa kufanya ushoga, kama njia ya kujipatia fedha, au ulaini wa maisha.
Mstaafu Askofu Mkuu Desmond Tutu, awali alitoa ushauri wake juu ya ushoga kwa Rais Museveni kwamba, historia ya binadamu imejaa majaribu mengi dhidi ya upendo au ndoa , na utengano kati ya matabaka na kimbali, lakini kisayansi hakuna msingi wa kubaguana kutokana na maumbile, bali katika upendo kuna tu neema ya Mungu.

Aidha mapema kabla ya Rais Museveni kuweka saini muswada huo , Kitengo cha Sheria za Wakimbizi katika Chuo Kikuu cha Makerere , kilisema, makundi ya utetezi wa haki za binadamu na wanaharakati, tayari walikuwa wakiathiriwa na muswada huo : baadhi ya watu binafsi na taasisi zilikuwa zikitishwa, kunyimwa haki yao ya kuwatetea mashoga. Vitengo hivyo vilimnukuu Wizara ya Afya nchini Uganda, akisema , hakuna sababu za kuwa na wasiwasi juu ya ushoga kwa kuwa ushoga umekuwepo katika historia ya taifa duniani.

Rais Museveni amepitisha sheria hiyo baada ya kikundi cha wanasayansi kumthibitishia kwamba, hakuna anayezawaliwa akiwa shoga, lakini zaidi sana hutokana na mtu kujiendekeza. Na kwamba alichelewa kuweka sahihi yake katika muswada kwa kuwa alikuwa akisubiri jibu la watalaam iwapo kuna wanaozaliwa wakiwa mashoga. Hakuna anayezaliwa na kilema cha ushoga.








All the contents on this site are copyrighted ©.