2014-02-25 11:19:55

Maaskofu wanashirikishana mang'amuzi kuhusu umoja, upendo na mshikamano miongoni mwa wafuasi wa Kristo!


Maaskofu Marafiki wa Chama cha Kitume cha Wafokolari kutoka Afrika, Asia, Mashariki ya Kati, Amerika na Ulaya wako mjini Castel Gandolfo wakiendelea kushirikishana: uzoefu na mang'amuzi ya umoja, upendo na mshikamano miongoni mwa wafuasi wa Yesu Kristo. Baadhi ya Maaskofu wanaotoka katika nchi ambazo bado kuna vita na kinzani za kijamii. Maaskofu wanashirikishana juu ya mchango wa Kanisa katika kukuza na kudumisha majadiliano ya kidini na kiekumene mintarafu changamoto za Uinjilishaji Mpya.

Baadhi ya viongozi wametoa mada inayogusia ufahamu wa Kanisa mintarafu mwono na maelekeo ya Baba Mtakatifu Francisko, mwaka mmoja tangu alipochaguliwa kuliongoza Kanisa Katoliki. Maaskofu wanaangalia pia umuhimu wa Sinodi za Maaskofu kadiri ya Mafundisho ya Papa Francisko.

Mkutano huu wa Maaskofu umefunguliwa rasmi hapo tarehe 24 Februari na utahitimishwa hapo tarehe 28 Februari 2014 baada ya kukutana na kuzungumza na Baba Mtakatifu Francisko, hapo tarehe 27 Februari 2014.







All the contents on this site are copyrighted ©.