(Vatican) Baba Mtakatifu Francisko , Jumamosi hii , ataongoza Mkutano wa Kawaida
wa Makardinali wa hadhara , majira ya saa tano za asubuhi , katika Kanisa Kuu la
Mtakatifu Petro, kwa nia ya kuwasimika Makardinali wapya 19, alio wateua hivi
karibuni. Maelezo yametolewa kwamba, kati ya makardinali hao wapya 16 wana umri
chini ya miaka 80, na hivyo wana haki ya kupiga kura katika kikao cha Makardinali
cha kumchagua Khalifa wa Mtume Petro kinacho julikana kama "Conclave", na pia haki
ya kuchaguliwa kukalia kiti hicho. Watatu wana umri zaidi ya miaka 80 na hivyo hawana
haki ya kuchagua au kuchaguliwa kuwa Papa. Kati ya kazi muhimu za Baraza la
Makardinali ni kumchagua Papa, lakini pia ni chombo cha ushauri cha kijadi ambacho
kinaweza kuitwa kama "seneti ya Papa. Hivyo Papa Francisko pamoja na kuitisha mkutano
wa Makardinali kwa nia ya kuwasimika Makardinali wapya, pia ameutumia uwepo wa Makardinali
hapa Vatican, kujadili baadhi ya vipaumbele vinavyo hitaji marekebisho ya haraka .
. Ifuatayo ni orodha ya Makardinali wapya na historia yao fupi katika utumishi
wa kanisa
Pietro PAROLIN Tangu mwaka 1986, alikuwa akitumika katika Idara
ya Diplomasia ya Jimbo la Papa, hadi mwaka 2009 alipo teuliwa kuwa mwakilishi wa
Papa nchini Venezuela . Na mwaka 2013, Papa Francisko alimteua kuwa Katibu wa Jimbo
Takatifu.
LORENZO BALDISSERI Aliwahi kuwa Nuncio wa Papa Brazil. Na alifanywa
kuwa Katibu wa Usharika wa Maaskofu Brazil, tangu January 2012 hadi alipoteuliwa
kuwa Katibu Mkuu wa Mkutano wa Sinodi ya Maaskofu iliyoitishwa na Papa Francisko Septemba
2013.
G erhard LUDWIG Muller Mwaka 2012 aliteuliwa kuwa Mkuu wa Shirika
kwa ajili ya Mafundisho Sadikifu ya Imani Katoliki, na pia Na Rais wa Tume ya Kanisa
la Mungu , na Rais wa Tume ya Kipapa kwa ajili ya Biblia na Rais wa Tume ya Kimataifa
ya Teolojia Ujeruman.
Beniamino STELLA Amekuwa katika Idara ya Diplomasia
ya Jimbo la Papa tangu mwaka 1970. Na hivi karibuni alikuwa ni Nunsio wa Papa nchini
Cuba nai Colombia,hadi Septemba 2013, alipo teuliwa na Papa Francisko kuwa Mkuu
wa shirika la ya Makreli Septemba 2013.
VINCENT GERARD NICHOLS Hadi
hivi karibuni alikuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki la England na Wales.
Ameisha pia kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Birmingham ( Uingereza ) kati ya Mwaka
2000 Rangi 2009, na baadaye kuteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Westminster ( Uingereza
) .
LEOPOLDO Jose BRENES SOLÓRZANO Aliteliwa na Papa Yohane Pauloo 11 kuwa
Askofu Mkuu wa Managua (Nicaragua) hapo Machi 2005.
Gerald Cyprien LaCroix
, I.S.P.X. amekuwa ni sehemu ya uongozi katika Taassii ya Papa Pio X, tangu Mwaka
1975,akiwa Katibu Mkuu na Mkurugenzi Mkuuu wa taasisi hiyo , na pia Mkurugenzi Mkuu
wa malezi ya kiroho wa jumuiya ya Uamusho mpya. Na aliteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa
Québec (Canada) na Papa Benedict XVI, Februari 2011.
Jean -Pierre Kutwa
Askofu Mkuu wa Gagnoa ( Ivory Coast) ,na tangu Mei 2006 aliteuliwa kuwa Askofu Mkuu
wa Jimbo Kuu la Abidjan ( Ivory Coast) Mei 2006.
ORANI Joao TEMPESTA , O.
cist . Aliteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa São Sebastião Rio de Janeiro (Brazil)
hapo Februari 2009
GUALTIERO BASSETTI Awali alikuwa ni mjumbe wa Tume ya
Maaskofu wa Italia kwa ajili ya Maisha ya Makreli na maisha yaliyowekwa wakfu. Na
pia mi mjumbe katika Bodi Katoliki kwa ajili ya Utamaduni na Ushirikiano na makanisa
ya Kiothodosi ya utamaduni wa Byzantine na Makanisa ya Mashariki ya Kiothodosi.
Kwa Sasa ni Makamu wa Rais wa Mkutano Maaskofu Italia, na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu
la Perugia - Città della Pieve (Italia) .
MARIO AURELIO PIOLI Kwa Sasa
ni Rais wa Tume ya Maaskofu kwa ajili ya Elimu Katoliki na Tume ya Maaskofu kwa ajili
ya shughuli za Idara za Baraza la Maaskofu Katoliki Argentina. Pia aliteuliwa kuwa
Askofu Mkuu wa Buenos Aires (Argentina) na Francisko Machi 2013.
ANDREW
YEOM soo - JUNG Askofu MKUU wa Seoul (Korea ya Kusini ) tangu Mei 2012. Awali
kwa mfululizo alitumikia katika nafasi mbalimbali za juu katika utawala wa Parokia
na seminari nchini Korea ya Kusini .
Riccardo EZZATI ANDRELLO , S.D.B. Msalesiani,
Awali alikuwa ni Askofu Mkuu wa MKUU wa Concepción (Chile) , na Desemba 2010 aliteuliwa
kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Askofu MKUU wa Santiago (Chile) katika Desemba 2010.
Philippe
NAKELLENTUBA Ouédraogo Hapo Awali alikuwa mjumbe katika Shirika kwa ajili ya Uinjilishaji
wa Watu, na kuteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Ouadraogo (Burkina Faso) na Papa Benedict
XVI, Mei 2009.
ORLANDO Quevedo, O.M.I. Mmisionari wa Oblates of
Mary Immaculate, aliteuliwa Askofu wa Kwanza wa Kidapawan (Philippines) baada ya
Jimbo jIpya kuundwa Novemba 1982, na baadaye kuteuliwa kuwa AskofuMkuu wa Jimbo
Kuu la Cotabato (Philippines) mwaka 1998.
CHIBLY Langlois Aliteuliwa kuwa
Askofu wa Les Cayes (Haiti) Agosti 2011. Awali alikuwa ni Profesa katika masuala
ya teolojia ya kichungaji katika semnari Kuu ya Mama Yetu ya Port- au -Prince (Haiti)
na pia Profesa katika Taasisi ya Jimbo Katoliki ya Elimu Binadamu ya Jacmel (Haiti)
.
LORIS Francesco Capovilla Mwandishi wa habari , na mhariri wa Zamani
wa gazeti la kila wiki la Venice ( Italia) , aliwahi pia kuwa Katibu wa Angelo Giuseppe
RONCALLI , baadaye Papa John XXIII. Na likuwa Mjumbe wa Papa katika Madhabahu Mataktifu
ya Loreto (Italia) tangu mwaka 1971 Hadi alipostaafu Mwaka 1988. Kwa sasa ana umri
wa miaka 98, atakuwa ni Askofu Mkuu mzee wa tatu duniani na pia anakuwa ni mzee kuliko
wote , katika decania ya Makardinali..
Sebastian AGUILAR , C.M.F. Mmisionari
wa Shirika la Moyo Safi wa Maria na awali alikuwa Askofu wa Leon ( Hispania ),na kwa
sasa ni Askofu Mkuu mstaafu wa Jimbo la Pamplona ( Hispania ), ambalo aliliongoza
tangu mwaka 1993 Hadi alipostaafu Mwaka 2007.
Kelvin EDWARD FELIX Aliwahi
kuwa Rais wa Baraza la Makanisa ya Caribbean, pia Mjumbe katika Baraza la Kipapa
kwa ajili ya ajili ya Mazungumzo na dini zingine, na pia ni Askofu Mkuu Mstaafu wa
Castries (Saint Lucia ) , ambako aliongoza Jimbo hilo tangu mwaka 1981 hadi alipostaafu
Mwaka 2008