2014-02-22 15:17:13

Hotuba ya Katibu wa Vatican kwa kikao cha Consistori: alikuwepo pia Papa Mstaafu Benedikto XV1.


Jumamosi hii , Ibada ya hadhara ya kikao cha kawaida cha Baraza la Makardinali, iliyo fanyika kwa nia ya kuwataja na kuwasimika Makardinali wapya 19, iliyo fanyika ndani ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican, Papa Msaatafu Benedikto XV1, pia likuwepo.

Papa Francisko kabla ya kuketi katika kiti chake alisalimiana na Papa Mstaafu Benedikto kwa upendo mkuu ndani, udugu wa Kristu. Papa pia alipeleka salam zake za matashi mema kwa Kardinali mpya Loris Francesco Capovilla, ambaye hakuweza kuhudhuria kikao hiki kutokana na hali ya afya kuwa teke.

Kikao kilifunguliwa na hotuba ya Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, ambaye alikuwa ni mmoja wa Makardinali waliosimikwa. Katika hotuba aliyoisoma kwa niaba ya Maaskofu na Makardinali wote,alitoa slaam za dhati kwake yeye Papa Francisko, na kwa Papa Mstaafu Benedikto XV1, na kwa pia alitoa salaam kwa Kardinali Loris Capovilla , ambaye hakuweza kuhudhuria tukio hili.

Aliendelea kumshukuru Papa Francisko kwa imani kubwa iliyo ionyesha kwao na wao wanatoa jibu lao kwa uaminifu, ukarimu na uvumilivu katika wito wao, ulio fumbatwa katika ishara ya vazi jekundu kama ishara ya kutenda kwa ujasiri, hata kama ni kupoteza maisha au kumwaga damu kwa ajili ya kuitetea Injili ya Kristu na kanisa lake Takatifu la Mitume na katika kuwaongoza na kuongeza Imani ya Kikristo, kwa amani na utulivu wa watu wa Mungu na kwa uhuru katika kulieneza Kanisa Takatifu Katoliki la Ulimwengu.


Na kwamba, kama mwanzo wa safari yao katika wito wa neema ya kuwa mfano bora kwa watu wote, wake kwa waume , ambao wamewasindikiza kwa namna mbalimbali za maisha ,alisema Katibu wa Vatican kwamba , wamepata neema ya kuelewa kwamba, kuwa mwanafunzi wa Yesu, ni kuugundua utakatifu na upendo , ambazo ni fadhila zisizo kuwa na kipimo na inaweza pia kudai zawadi ya maisha - kama ilivyotokea na inaendelea kutokea kwa Wakristo wengi katika dunia, na hivyo inakuwa ni jambo la lazima kutangaza hadharani, kuridhia wito huu .

Na wanatambua kwamba, kuwa Kardinali ni kuwa mjumbe na mhudumu wa kanisa hata wakati wa matatizo, vipingamizi na vishawishi vingi, daima ni kuubeba msalaba na kufuata mfano wa Mwana wa Mungu , aliyekuja kukaa kati yetu kama mtumishi (cf. Lk 22: 0.25-27 ) . Ni kufuata nyayo zake na kwa majitoleo binafsi kwa ajili ya upendo wake , na kwa unyenyekevu mkuu kwa Kanisa bibi harusi wake, na juu ya Msalaba. '

Katibu wa Vatican, alieleza na kurejea maneno ya Papa Mstaafu Benedict, kwamba, mbegu ya ngano iliyo shuka kutoka kwa Baba hadi shamba la dunia , aiikufa kwa ajili ya kuleta matunda y amaridhiano.

Na hivyo , kuianza kazi hii mpya katika Chuo cha Makardinali, ina maana ya kutenda vyema zaidi na kuwa wasaidizi wa Papa maalum , wakiwa katika umoja zaidi katika Kanisa la Ulimwengu , katika huduma ya ukarimu, wema na mashahidi wa Umoja wa Kanisa na katika mpanuko wake , unaofanikishwa na hamu mpya ya utendaji maalum wa kitume, waliokabidhiwa kwao , na katika idara za Curia ya Roma na Makao makuu ya Mabaraza ya Maaskofu mbalimbali.


Kardinali Mpya kwa niaba ya wenzake wote alikiri ushirikiano, kutembea na kuishi pamoja chini ya maongozi ya Baba Mtakatifu Francisko katika safari ya umoja wa uongofu wa kichungaji,na kitume, bila kuiachia hali ya dunia kwenda kama inavyotaka, bali kufanikisha katika mikoa yote, utume wa kudumu kwa mujibu wa mafundisho ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican ( Angalia EG 25).


Hotuba ya Kardinali Parolin, ilimhakikishia Papa Francisko, maombi yao kwa Mama Maria, Mama wa Mungu na Kanisa na Malkia wa Mitume. Pamoja na Mtakatifu Yosef, wenye Heri Yohane Paulo II, na Yohane XXIII,na watakatifu wote kwa maombezi yao kwa ajili ya Baba Mtakatifu , na kw ajili ya wote waliokuwa katika Ibada hii na Kanisa zima na dunia kwa ujumla.







All the contents on this site are copyrighted ©.