Sakramenti ya Kipaimara inawapatia waamini nguvu ya ya kulinda na kueneza Injili kwa
ujasiri mkuu!
Kwa pamoja na Ubatizo na Ekaristi Takatifu, Sakramenti ya Kipaimara hufanya Sakramenti
za kuingizwa katika Ukristo, ambao umoja wao lazima uhifadhiwe. Waamini wanapaswa
kutambua kwamba, kupokea Sakramenti ya Kipaimara ni lazima ili kukamilisha neema ya
Ubatizo.
Kwa njia ya Sakramenti ya Kipaimara muungano wa Wabatizwa na Kanisa
hufanywa kuwa mkamilifu zaidi, kwani wanatarajirishwa kwa nguvu ya pekee ya Roho Mtakatifu
na hivi hulazimika kwa nguvu zaidi kuieneza na kuitetea imani kwa maneno na matendo
kama mashahidi wa kweli wa Kristo!
Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake
kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anawakumbusha kwa mara nyingine tena umuhimu
wa Sakramenti ya Kipaimara kwa Mkristo. Hii ni Sakramenti inayowakirimia nguvu ya
kulinda na kueneza Injili kwa ujasiri mkuu.