2014-02-21 12:03:57

Papa akutana na kikundi cha wafungwa toka magereza la Pisa na Pianosa.


Jumatano Papa akiwa katika makazi yake kwenye jengo la Mtakatifu Marta alikutana na kikundi cha wafungwa, wapatao 19, kutoka Magereza Pisa na Pianosa , kabla hajaenda kutoa katekesi yake kwa mahujaji na wageni waliokuwa wamejumuika katika uwanja wa kanisa kuu la Mtakatifu Petro.

Papa akiwa na wafungwa hao , alisali pamoja nao, mbele ya sanamu ya Bikira Maria Mama Yetu, mwenye kufungua vifundo vyote vya kifungo , ambaye Papa humheshimu kwa namna ya kipekee . Na baada ya sala , aliwasamia wafungwa hao na kuwasikiliza mmoja baada ya mwingine . Na kwa mfungwa mmoja alimpatia barua yake ya kichungaji ambamo mna maneno ya huruma na msamaha.

Katika mazingira ya kiroho , wafungwa hao walikuwa wamesindikizwa na Mapadre wawili, Padre Roberto Filippini, na Padre Luigi Gabriellini, na walihudhuria Ibada ya Misa, iliyofanyika katika mapango ya ndani ya Vatican, majira ya saa moja za asubuhi.
Na kwamba, Askofu Mkuu Lorenzo Baldisseri, alitoa taarifa kwa Papa , uwepo wa wafungwa hao Vatican, na Papa alionyesha furaha ya kutaka kukutana nao yeye mwenyewe. Na hivyo walipekwa katika jengo la makazi ya Papa majira ya saa tatu na kukutana na Papa kwa kwa muda wa zaidi ya dakika 40 . Alikuwepo pia Mkurugenzi wa Idara ya Kitubio wa Jimbo la Pianosa , pia baadhi ya mawakili wanao wafuatiliaji wafungwa , walinzi wa Magereza, na wahudumu wengine wa kiroho.

Askofu Mkuu wa Baldisseri ameeleza kukutana kwao na Papa Francisko kuwa ni tukio kuu, lililowazamisha katika matumaini na imani , wakipata furaha za kusonga mbele kwa imani na matumaini. Na kwamba kwao imebaki daima kuwa ishara ya unyenyekevu na heshima ya Khalifa wa Mtume Petro katika kukutana na watu wote kuwaimarisha kiroho.








All the contents on this site are copyrighted ©.