2014-02-21 15:13:16

Hotuba ya Papa kwa Kikao cha Ijumaa asubuhi cha Consistori


(Vatican ) Papa Francisko , mapema Ijumaa hii , alitoa hotuba fupi kwa washiriki wa Mkutano wa Consistori, unaojadili mada ya familia, kabla ya kikao maalum cha Jumamosi ambacho kitakuwa na tukio la kuwasimika Makardinali wapya 19.
Hotuba hii ya Papa ,mapema Ijumaa kwa Mkutano huu, kwa namna ya kipekee, Papa alitoa salam zake kwa Makardinali toka Ukraina wanaoshiriki katika mkutano huu , katika mwanga wa machafuko yanayoendelea katika nchi yao. Papa pia alitoa maneno ya sifa kwa maandishi ya kiteolojia ya Kardinali Walter Kasper , Rais Mstaafu wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya kukuza Umoja wa Wakristu.








All the contents on this site are copyrighted ©.