2014-02-20 08:26:08

Siku ya tatu mkutano kwa ajili ya Baraza la Makardinali


(Vatican ) Padre Federico Lombardi, SJ , Mkurugenzi wa Ofisi ya habari ya Vatican, Jumatano, alitoa Muhtasari kwa wanahabari juu ya Mkutano wa Baraza la Makardinali 8 ambao ulifanyika Jumanne mchana.

Padre Lombardi ameeleza kwamba, kuna waandishi wa habari wengi wa kigeni walio wasili mjini Roma, kufuatilia mkutano wa Makardinali wa “Consistori” utakao fanyika mwishoni mwa wiki . Na kwamba Jumanne alasiri, Mkutano wa Makardinali Wanane , uliendelea na kazi yake, na ulipokea ripoti kutoka Tume ya Rejea ya Shirika la Uchumi –MiundoTawala katika Kiti Kitakatifu ( COSEA ).

Padre Lombardi alieleza kuwa, kutokana na matokeo ya taarifa hizo, Makardinali hao wanaandaa mapendekezo yao watakayo yasilishwa kwa Baba Mtakatifu.

Aliendelea kuweka bayana kwamba, mchakato huu hasa unalenga taasisi ya Vatican inayo husiana na masuala ya uchumi na fedha, na Mashirika ya Katoliki ( IOR ) , inayojulikana kama Benki ya Vatican. Na kwamba, ingawa Makardinali wameandika mapendekezo yao, kwa mujibu wa tathmini yao wenyewe, mwenye kutoa maamuzi ya mwisho ni Papa mwenyewe.
Aidha Padre Lombardi alisema, mchana Jumatano , Makardinali 15 wajumbe wa Mkutano wa Baraza la maandalizi ya Kikao cha Consistori tayari wamewasili Vatican kwa maandalizi yao. Na kwamba wao pia watapokea ripoti za Tume mbili zilizotajwa hapo juu.







All the contents on this site are copyrighted ©.