2014-02-20 12:24:27

Lindeni ukweli na uhalisia wa Liturujia


(Vatican )Katibu mkuu wa Vatican, Askofu Mkuu Pietro Parolin, ametoa wito wa kulinda na kudumisha mapokeo ya liturujia na kufungua mlango wa neema ambayo yenye ina uwezo wa kujipandikiza na kuhifadhi ukweli wake. Hili alilieleza katika homilia yake, wakati wa Misa iliyo iongoza Jmanne asubuhi katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Ibada hii ilikuwa ni sehemu ya Mkutano unaoendelea katika Kanisa kuu la Lateran , juu ya Maendeleo ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican (Katiba ya Vatican II)toleo la mwaka wa 1963, lillilo fanya mabadiliko makubwa katika Liturujia ya Kanisa.

Askofu Mkuu Parolin amesema , Mtaguso huo ni "Hema" ambamo Mungu na mtu hukutana. Ni njia iliyo daima wazi ambayo huleta Roho Mtakatifu kutoka mbinguni hadi duniani. Kwa miaka elfu mbili, fikra za Kikristo zimepata maneno mengi kuelezea umuhimu wa Liturujia ya Ekaristi. Na kwa miaka 51, ya Katiba ya Sacrosanctum Concilium, ni shara na kazi inayowasilisha Uakatifu wa Mungu katika ubinadamu.
Liturujia , amesema Askofu Mkuu Parolin , inaruhusu utakaso wa mwanadamu kwa njia ya "ishara za neema katika hatua ya kufanya nafasi mpya ,kwa ajili ya maisha ya ukombozi. Daima jambo hili hushangaza, mara paleinapojidhihirisha katika hali ya unyenyekevu . Maisha ya Utatu Mtakatifu tunaoupokea kupitia maji ya Ubatizo , Mungu anajitolea kama chakula katika Ekaristi, na msamaha wake kwetu kwa njia ya ishara na maneno ya kikuhani :

Askofu Mkuu Parolin alikamilisha homilia yake akisema, siri ya maisha ya Kristo , imemwilishwa katika maisha ya kiroho ya Kanisa,na Liturujia inakuwa daima ni njia ya wazi na iliyojaa maji safi ambayo hutoka katika chemchemi ya Pasaka ,siri ya Kristu. Liturujia hulinda na kufungua mlango wa neema na huendelea kupandikiza na kutunza katika ukweli wake na madhumuni yake ya kweli.










All the contents on this site are copyrighted ©.