Jumuiya ya Mtakatifu Egidio yazindua ombi dhidi ya unyanyasaji
Mkutano wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidi wazindua ombi dhidi ya unyanyasaji wa binadamu
na tafakari: Je, dini zinaweza kukomesha unyanyasaji dhidi ya binadamu? Swali hilo
limetolewa kwa viongozi wa dini zote, wakitakiwa kutoa kutoa jibu sahihi kwa mujibu
wa imani yao.
Swali hilo ni hoja iliyojadiliwa katika mkutano ulioandaliwa
na Jumuiya ya Mtakatifu 'Egidio , kutazama mahusianao yaliyopo kati ya “Dini na Vurugu”
, ambao ulihudhuriwa na wajumbebe kutoka dini kuu tatu, Wakristu , Wayahudi na
Waislamu, pamoja na mabalozi , wasomi na wachambuzi wa mambo.
Sabatinelli
wa Redio Vatican akitaarifu tokea mkutano huo ametaja kati ya waliohudhuria mkutano
huu ni Kardinali Walter Kasper , Rais Mstaafu wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Umoja
wa Wakristu. Hotuba yake kwa mkutano huu ilileleza kwamba uhafidhini na ugaidi ni
mambo yanayaweza kuchafua dini , na kuifanya dini kuwa tena si chombo cha kueneza
amani bali vifo. Kardinali alieleza hayo akitazama baadhi ya migogoro iliyopo sasa
sehemu mbalimbali za dunia , maeneo ya Afrika , Mashariki ya Kati , na Asia. Vurugu
nyingi zinazofanywa kwa kisingizio cha kulinda haki za kidini kwa kutumia vurugu.
Kardinali Walter Kasper alisema, kama ilivyokwisha elezwa katika mikutano
mingine ya Jumuiya ya Mtakatifu Egidio hapa Roma , licha ya tofauti za mafundisho
na mapokeo ya kidini, ilithibitishwa kwamba, hakuna dini inayo halalisha vitendo
vya unyanyasaji, vurugu na mauaji. Na jina la Mungu haliwezi kutumiwa kuhalalisha
ugaidi. Na kwamba ni lazima na hawawezi kusahau kwamba, kuna watu wanaoteseka na
kuathirika kwa sababu ya imani yao, wakiwemo Wakristo . Hivyo, kama viongozi wa kidini,
hawawezi kukwepa uchunguzi wa dhamiri, na wajibu wa kukemea vikali utendaji wowote
unaolenga kuvuruga mahusiano mazuri kati ya dini na hasa kwa kati ya dini zinazoamini
katika Mungu mmoja.
Karidinali Walter Kasper aliendelea kueleza kwamba, leo
kuna matumizi haya mabaya ya dini ambayo mara nyingi imekuwa kisingizio cha machafuko.
Lakini ukweli wa machafuko hayo ni sababu au maslahi ya kiuchumi , kisiasa, kijamii.
Na inapaswa kukumbukwa na wote kwamba, dini ni kwa ajili ya amani , amani ambalo
ni jina la Mungu, na kwa hiyo dini anatuita katika kuwa na amani , kuthamini na
kumtambua mtu mwingine,kuwa pia ameumbwa kwa mfano wa Mungu . Kusadiki hilo ni kuitakatifusha
dini na fikira zinazo lenga katika kiini cha dini na moyo wa kubadilika , na kuwa
na mtu wa amani , yaani kuishi na Mungu ndani ya moyo. Ni kuwa na amani ya kweli itokayo
moyoni .
Na Abdelfatah Mourou , Makamu wa Rais wa chama cha Ennahdha Tunisia,
na mwandishi wa Katiba mpya, amehoji iwapo vurugu na manyanyaso yamevaa mavazi ya
dini nyenye kukiuka haki za binadamu, ambayo hakuna tena haki katika kiuchumi,
heshima kwa haki za kijamii na kisiasa. Na iwapo jina la Mungu yaani amani linatumika
katika maana yake halisi? Kwa swali hilo, alisema , Jibu ni lazima kila kiongozi
wa dini ahubiri umuhimu wa kuachana na unyanyasaji na vurugu, kwa sababu hakuna dini
inayofundisha udikteta, au mawazo ya kibaguzi, au ubinafsi kiuchumi , na masuala
mengine yanayo sababisha shida za kijamii. Watu wanahitaji zaidi haki kutekelezwa
. Kupotoshwa kwa nia za kidini na haki hasa na viongozi , ndiyo chanzo cha vurugu
na manyanyaso yanayo jitokeza sasa. Na Andrea Ricardi, Mwanzilishi wa Jumuiya
ya Mtakatifu Egidio amesema , hakuna dini inayo tetea vurugu, vurugu zinazo tokea
ni majaribu makali dhidi ya dini,hivyo yanayohitaji uponyaji wa ndani ya roho.