Hotuba ya Papa kwa kikao Maalum cha Baraza la Makardinali Vatican
Makardinali wote wamekusanyika mjini Vatican kwa ajili ya kikao maalum cha Baraza
la Makardinali kinachojulikana kama "Consistori", kilichoanza mapema asubuhi ya Alhamis
hii mjini Vatican, ambamo Jumamosi ijayo, Makardinali wapya 19 waliotajwa na Papa
hivi karibuni , watafanywa kuwa Makardnali..
Papa katika salaam zake kwa
Makardinali, amewaomba Makardinali wote, kuzamisha mawazo yao katika umuhimu wa kuweka
mbele uzuri wa familia na ukuu wa ndoa , kweli ya maisha ya binadamu, ambayo huonekana
kuwa mepesi , lakini ndani mwake mmejaa utajiri mwingi wa furaha na matumaini, mapambano
na mateso, kama sehemu ya maisha . Na kwamba, katika kikao hiki wanatafuta kuzama
zaidi katika misingi ya kiteolojia juu ya familia na kutambua shughuli za kichungaji
katika mahitaji ya mazingira ya wakati huu.
Papa ameeleza na kurejea historia
ya binadamu kwamba, tangu mwanzo, Muumba alimbariki mwanamume na mwanamke ili wapate
kuzaa, kuongezeka na hivyo hivyo kuwa na familia katika mfano wa Utatu wa Mungu
duniani .
Papa amewataka Makardinali kutekeleza hayo lakini wakiwa makini na
bila ya ugandamizaji, pia bila ya kupoteza onjo na ubora kazi zao za kichungaji.
Leo hii Papa ameasa , familia inaonekana kupuuzwa na kunyanyaswa. Hivyo wao kama
viongozi wa kanisa, wanatakiwa kukiri uzuri na ukweli na jinsi ilivyo vyema kuanza
familia leo hii , na jinsi familia ilivyo ya lazima kwa maisha ya dunia na binadamu
wa baadaye. Na kwamba, wameitwa kuufankisha mpango mkubwa wa Mungu kwa ajili ya
familia na kusaidia wanandoa kuishi kwa furaha mpango huu katika maisha yao, na kuongozana
na wanadoa katika matatizoyao mengi .
Papa alikamilisha hotuba yake kwa kumshukuru
Kardinali Walter Kasper kwa mchango wake muhimu .