2014-02-19 16:14:11

Kila tunapokiri dhambi;Mungu hutukumbatia -Papa


Baba Mtakatifu mapema Jumatano, ametoa Katekesi kwa mahujaji na wageni waliokuwa wamekusanyika katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, kama ilivyokuwa kawaida ya siku hii. Katika maelezo yake , ameangalisha katika Sakramenti ya Ubatizo ambao ni mwanzo wa mtu kuwa Mkristu, akisema, kwa njia ya Sakramenti za kwanza za Ukristu , ubatizo , Ekaristi na Kipaimara , mtu anapata maisha mapya katika Kristo. Na baada ya hapo Wakristu wanapaswa kutambua kwamba, sasa ndiyo wanaianza safari ya maisha ya kweli ambayo si lele mama "(2 Kor 4:07 ), lakini ni maisha yaliyojaa majaribu, mateso, na hata mauti, kwa sababu ya dhambi ya asili , na bila kuwa waangalifu maisha haya mapya hata wanaweza kuyapoteza.

Kwa sababu hii Papa amefafanua, Bwana Yesu alitaka Kanisa liwe pia na Sakramenti nyingine sakramenti ya msamaha wa dhambi (upatanisho) au kitubio na mpako wa mafuta ya wagonjwa , ambavyo vinaweza kuwa chini ya jina la moja " sakramenti za uponyaji" .
Papa Francisko ameendelea kufundisha kwamba, Sakramenti ya Upatanisho ni sakramenti ya uponyaji. Na wakati muumini anapokwenda kukiri dhambi zake mbele ya kuhani, anakwenda kuomba kuponywa roho , kuponya moyo wake kwa kila jambo lililoichafua roho. Papa ameeleza kwa kurejea mfano unao onyesha dhamana bora ya kina katika msamaha na uponyaji wa mtu aliyepooza, ambapo Yesu alifanya yote mawili kwa wakati mmoja , kama daktari wa mwili na kiroho. (cf. Mk 2:1-12 / / Mt 9,1-8 , Lk 5.17-26 ).

Papa aliendelea kuizungumzia Sakramenti yaKitubio na Upatanisho ambayo pia huitwa sakramenti ya maungamo,akisema tunaweza kuiunganisha moja kwa moja na fumbo la Pasaka . Kwa kweli, usiku huo wa Pasaka, Bwana alijitokeza kwa wanafunzi katika chumba ghorofani kilicho kuwa kimefungwa, na , baada ya salamu "Amani iwe nanyi" , akawavuvia na kuwaambia , " Pokeeni Roho Mtakatifu. Kwa wale ambao mtawasamehe dhambi zao nao watasamehewa "(Yn 20:21-23) .
Papa amesema, kifungu hiki , kinaonyesha zaidi utendaji wa ndani wa Sakramenti. Awali ya yote, ni ukweli kwamba, msamaha wa dhambi zetu si jambo tunaloweza sisi kujipa wenyewe, katika maana ya kujiondolea dhambi mwenyewe , mimi nimejisamehe dhambi zangu, lakini msamaha unadai kutolewa na mtu mwingine, na kuomba msamaha ni kuomba na kumkiri Yesu kuw andiye mwenye kuondoa dhambi na si mtu mwingine. Na msahama si matokeo ya juhudi zetu , lakini ni zawadi, ni zawadi ya Roho Mtakatifu , ambaye anatujaza na kututakasa kwa huruma na neema inayotoka kwa Yesu Kristu Msulubiwa na Mfufuka, alieyufunua moyo wake wote wazi kwa ajili ya kusamehe wadhambi bila ukomo.
Papa amekubusha kwamba, kujipatanisha na Baba wa Mbinguni, na Bwana Yesu Kristo na ndugu zetu, tunakuwa na amani ya kweli. Na hili huweza kusikika ndani ya mioyo ya wote wale wanaoiendelea altare ya maungamo , wakiwa wamejawa na moyo mzito na woga lakini mara wanaposiki Yesu amewasamehe dhambi zao, mara hujisikia wepesi moyoni na kuwa na amani zaidi.
Papa ameendelea kufundisha kwamba , kuiadhimisha Sakramenti ya Upatanisho maana yake ni kuikumbatia kwa nguvu , kukumbatia bila ukomo huruma ya Baba. , kama ilivyokuwa kwa mfano wa Mwana Mpotevu aliyetapanya sehemu ya urithi na baada ya kuishiwa, dhiki kubwa ilimfanya arudi nyumbani kwa aibu , si kama mtoto lakini kama mtumishi . Moyoni mwake alijisikia vibaya sana na alijiona kuw na hatia moyoni mwake na kushikwa na aibu kubwa . Lakini kwa mshangao wakati yeye akianza kuzungumza na kuomba msamaha kwa Baba yake, alimkubatia na kumbusu kwa huruma na kumkaribisha nyumbani, si kama mtumishi lakini kama mtoto.
Papa anasema maajabu haya. Na ndivyo Mungu anavyotutendea sisi tunapojitenga nae na kutapanya baraka alizotujalia , tukijichafua kwa dhambi, mara tunapomrudia yeye hutukumbatia na kutubariki tena, kama wana wake. Tunachotakiwa kila mara ni kurejea katika madhabahu ya kitubio na upatanisho kusema baba nimekosa , naye kwa wingi wa huruma atatupokea na kutukumbatia na kutupatia tena baraka zake. Baada ya salaam zake Papa alisalimia katika lugha mbalimbali. Wiki hii makundi makubwa ya mahujaji na wageni walitoka Uingereza , Norway, Nigeria , Japan na Marekani.








All the contents on this site are copyrighted ©.