2014-02-18 09:18:33

Kenya kwaanzishwa chama cha Muziki wa Liturujia


Kwa ajili ya kukuza ubora wa muziki na nyimbo za kiliturujia, katika makanisa Kenya kulingana pia na kuthamini mambo ya utamaduni wa wenyeji, kumeanzishwa chama kipya cha muziki wa Kiliturujia. Mvuto wa muziki wa kiliturujia ni wazo msingi nyuma ya juhudi za kuanzisha chama hicho kipya cha Muziki Katoliki wa kiliturujia nchini Kenya ( Catholic Liturugical Music Association of Kenya - Clmak ) kwa idhinishi ya Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya, katika mwanga wa kukuza uhai wa vivutio katika Ibada.
Kwa mujibu wa CISA, wakati wa Ibada ya Ekaristi iliyo fanyika mjni Nairobi, Rais wa Tume ya Maaskofu kwa ajili ya Lituruijia , Askofu Dominic Kimengich , aliwasilisha chama kipya cha Muziki wa Kiliturujia wakati wa hotuba yake. Aliwashukuru Maaskofu kwa kutoa idhini yao kwa mpango huo, unaoelnga kutumika katika kuongeza onjo kwenye muziki na nyimbo za Ibada zinazo fanikishwa na vipaji vya waamini. Hata hivyo alisema , bado kuna mengi ya kufanyika, kutokana na kwamba mengi wanayanakiri kutoka kwa wengine na hivyo nyimbo na muziki wao wakati mwingine hauipatani sana, kati ya maneno na vyombo vya ala.
Askofu Kimengich, alitaja umuhimu wa muziki katika ibada kwamba, ni lazima kuonyesha msingi wa mafundisho ya Mapapa, na yaliyomo katika hati ya Mtaguso Mkuu wa pili wa Vatican, " Sacrosanctum Concilium " juu ya Muziki Mtakatifu wa Liturujia , ambao hutukumbusha kwamba " utamaduni muziki wa Kanisa Katoliki, ni hazina ya thamani sana, zaidi ya hata kuliko ile ya sanaa nyingine yoyote, hasa kwa ukweli kwamba wimbo Mtakatifu , katika muungano wa maneno , unakuwa na muhimu wake kama sehemu ya Liturujia Takatifu. Papa Mstaafu Benedikto XV1, pia alionyesha mapezi makubwa katika umuhimu wa muziki Mtakatifu , wakati akizungumza na Chama cha Muziki cha Mtakatifu Cecilia cha Italia hapo , Novemba 10, 2012, alisema hivi: " muziki wa kiliturujia si tu nyongeza au pambo la nje ya Liturujia , lakini ni sehemu ya ibada hiyo ".








All the contents on this site are copyrighted ©.