2014-02-18 10:47:57

Kardinali Ruini :waumini wapambana na mashinikizo ya kijamii na vikwazo


(Roma)Kardinali Camillo Ruini , Rais wa Shirika la Hija la Italia (Opera Romana Pellegrinaggi (ORP) ) amesema katika miaka ya hivi karibuni waumini wanakiishi kishindo cha nguvu za mashinikizo ya mazingira ya kijamii na kitamaduni , ambayo hutoa mtazamo kwamba, maisha ya Kikristo ni kama vile yamepitwa na wakati wala si maisha endelevu.

Mashinikizo yanayowafanya Wakristu kujisikia kama vile ni waathirika wa mambo ya kale yaliyopitwa na wakati . Lakini Wakristu wanapaswa kuendelea na utambuzi wao kwamba imani haipitwi na wakati, bali ni maisha endelevu yenye furaha kamili na nafasi ya kupumua anga tofauti . Hayo yaliyaeleza siku ya Jumapili mjini Roma , katika hotuba yake ya uzinduzi wa Mkutano wa Kazi za Kichungaji zha Teolojia kwa ajili ya ajili ya maadhimisho ya 80 ya hija Shirika la ORP . Kardinali Ruini alikuwa Rais wa Orp, tangu wakati akiwa Vika wa Jimbo la Roma miaka ya nyuma.

Shirika la habari la SIR – limeripoti kwamba, Kardinali alizungumzia haja ya kuwa na wakati na nafasi tofauti, kwa ajili ya kupumua hewa tofuati kama vile kuwa na vipindi vya tafakari za kiroho na Hija katika moja ya maeneo Matakatifu, kama ilivyo ilivyojionyesha katika uzoefu na upembuzi yakinifu kwa watu wengi, hata miongoni mwa wale ambao huwa hawahudhurii Ibada kanisani mara kwa mara. Na pia Hija, aliendelea – huweza kuwaweka pamoja vijana na wazee na wengine wasiokuwa na mazoea ya kumcha Mungu .

Kardinali ametaja kati ya siri ya hija iliyonzuri zaidi , ni upatikanaji wa viongozi wazuri si tu katika kuzungumza na kuhubiri vizuri, lakini pia kusikiliza maoni ya wanahija kwa muda mrefu, mbali na uwepo wa majadiliano katika makundi madogo madogo juu ya masuala ya kileo na ya ushawishi wa mashinikizo ya jamii dhidi ya waamini leo .

Na aliongeza kutafakari juu ya asili ya Hija, akibainisha kuwa , katika mchakato wa mapenzi kwa malimwengu na ukana Mungu , unao ongeza pia kukua kwa wimbi jingine: la ubinafsi wa kidini. Watu wengi wanaamini katika Mungu , na mara nyingi hata kwa Yesu Kristu, na labda huomba, lakini wakipendelea kufanya hivyo kama mtu mwenyewe binafsi, bila ya kujiunga na jumuiya yoyote ya Kikristu. Na sababu zinazotajwa na watu wa namna hiyo, mara nyingi ni jeuri ya ubinafsi , wa mtu kutotaka kuingiliwa akiona kama anajitosheleza mwenyewe, hivyo husema Yesu ndiyo, Kanisa

Katika mzamo huo, hija inaweza kuwa tukio la kusaidia mtu wa namna hiyo, kugundua upya , furaha na nafasi ya mpya ktika uzoefu wa maisha, manufaa ya kujumuika pamoja kama watu wa imani moja kutolea sala na maombi , ambayo kiini chake ni mkusanyiko ndani ya Kanisa zaidi ya kuthamini tu mikusanyiko ya pamoja katika masuala ya kidunia, nguvu ya kiuchumi, na kisiasa, na hali halisi au bandia , ambayo daima hupendelewa na vyombo vya habari.

Kwa mujibu wa Kardinali Ruini, Hija ni fursa nzuri ya kujaribu kushinda na utengano kizani au mbadala hewa, unaonekana mara kwa mara katika sala ya binafsi na sala ya pamoja ya waamini. Ibada zinazofanyika wakti wa Hija amesisitiza , zinapaswa kukuza umoja njia vizuri zaidi ya kuleta mwamko wa kuhudhuria pia ibada za Misa za siku ya Jumapili , katika parokia.

Kardinali Ruini amekamilisha kwa kugusia mada inayogusa katika mtima wa utamaduni wa leo ambamo watu kuwa na hisia za kutokuwa na dhambi. Amesema hisia hizi ni kinagusa kiini asilia cha utamaduni na mawazo , ambayo dhamiri au hisia ya dhambi inakuw ani ugonjwa wenye kuhitaji kuponywa na kujikwamua . Kwa mujibu wa Kardinali, kugundua zaidi juu ya "hisia ya dhambi" inaweza kutokea wakati wa Hija. Hija huwakilisha mwanzo wa njia mapya, ya maisha ya watu wengi ambao pengine kwa muda mrefu wamekuwa mbali na Kanisa.







All the contents on this site are copyrighted ©.