Kukosa na kukoseana ni sehemu ya ubinadamu; kusamehe na kusahau ni kuanza hija ya
utakatifu wa maisha. Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa
mitandao ya kijamii anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema kujifunza kutoka
kwa Kristo jinsi ya kusali vyema; kusamehe na kupandikiza mbegu ya amani.
Waamini
wajifunze kujenga na kuimarisha mshikamano na maskini pamoja na wote wanaosukumizwa
pembezoni mwa Jamii.