Guinea kuendelea kupata msaada wa fedha kutoka IMF
Shirika la Fedha Duniani, IMF limeamua kuendelea kufadhili miradi mbali mbali ya maendeleo
nchini Guinea iliyokuwa imebainishwa na Shirika hili mwaka mmoja uliopita. Licha ya
hali ngumu ya kisiasa na kijamii, lakini bado wananchi wengi wa Guinea wanakabiliana
na hali ngumu ya uchumi unaosababishwa na umaskini mkubwa kati ya wananchi wake.
Kuna
baadhi ya wananchi wa Guinea wanaishi chini ya wastani wa dolla moja ya kimarekani
kwa siku. Shirika la Fedha Duniani linaonesha kwamba, uchumi wa Guinea kwa Mwaka 2013
umekuwa kwa asilimia 2.5 kichume cha asilimia 4.5 kilichokuwa kimekadiriwa kwa Mwaka
huo. Mfumuko wa bei ya bidhaa na huduma umepungua lakini bado ni wa kiwango cha juu.
Shirika la Fedha Duniani limetoa kiasi cha dolla millioni 28. 2. Katika kipindi cha
miaka mitatu, IFM itachangia kiasi cha dolla za kimarekani millioni 112. 8 za Kimarekani.