Boko haramu inaendelea kusababisha majanga nchini Nigeria
Askofu mkuu Ignatius Ayau Kaigama, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Nigeria anasema,
mashumbulizi yaliyotokea nchini Nigeria hivi karibuni na kusababisha zaidi ya watu
mia moja kupoteza maisha hayakuwashangaza kwani hii ni kampeni chafu inayofanywa na
kikundi cha kigaidi cha Boko Haram kutaka kuwatisha na kuwajengea wananchi hofu isiyokuwa
na msingi.
Askofu mkuu Kaigama anasema, inasikitisha kuona kwamba, Serikali
na vyombo vya ulinzi na usalam bado havijafanikiwa kulinda na kutunza amani na utulivu
wa wananchi wa Nigeria. Serikali imewekeza kiasi kikubwa cha rasilimali fedha na watu,
lakini bado wananchi wasiokuwa na hatia wanaendelea kupoteza maisha yao kutokana na
mashambulizi ya kigaidi.
Kuna haja kwa Nigeria kutafuta sababu msingi ili
kuondokana na mashambulizi ya mara kwa mara yanayosababishwa na kiundi cha kigaidi
cha Boko Haram nchini Nigeria. Inawezekana kwamba, kuna mtandao mkubwa wa kigaidi
unaotekeleza lamelngo yake nje ya Nigeria anasema Askofu mkuu Ignatius Ayau Kaigama,
Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Nigeria.