Ziara ya nne ya Papa kutembelea Parokia Jimboni Roma.
Baba Mtakatifu Francisko , Jumapili iliyopita majira ya jioni alifanya ziara ya Kichungaji
katika Parokia ya Mtakatifu Thomas Mtume iliyoko nje kidogo ya jiji la Roma, kwa nia
ya kuvuvia na kuhamasisha uhusiano ukweli, uaminifu, na usafi wa moyo. Pia kutabaruki
Kanisa Jipya katika eneo hilo. Kwa ajili hiyo, Papa aliongoza Ibada ya Misa iliyohudhuriwa
na maelfu ya wakazi wa eneo hilo la Infernetto, Parokia ya Kusini mwa jiji la Roma
ambayo ni sehemu ya Jimbo la Roma.
Papa katika Parokia hiyo alikaribishwa
na umati mkubwa wa waaamini wakiongozwa na Kardinali Agostino Vallini , Vika wa Jimbo
la Roma, akiwepo pia , Askofu msaidizi wa eneo hilo, Msgr Paolino Schiavon na Paroko
Antonio D' Errico.
Akiwa katika Parokia hiyo, Papa alisalimiana na watoto
na kuwapatia kile kilichiiotwa tiketi ya kuanza safari ya kutembea katika imani,
akiwaambia siri ya kumpenda Yesu ni kumwachia yeye afanye kazi katika maisha yetu.
Kwa kuwa Yeye alitupenda kwanza. Watoto hao wadogo wakiwa na nyuso za tabasamu waliinyosha
mikono yao kwa Papa , huku wakisema, "Wewe ni rafiki yetu , na baadhi walipiga nae
tano, Kisha alikutana na wazazi wa watoto waliobatizwa hivi karibuni wazee, wagonjwa
, mapadre, na Chama cha Familia cha watoto wenye ulemavu. Na kabla ya Misa, alipata
muda wa kuwaungamisha waaamini kadhaa.
Wakati wa Ibada , Papa aliangalisha
homilia yake, katika somo la Injili , ambamo Mtakatifu Matayo anahimiza uhusiano
mzuri kati ya mtu na mtu na hasa katika maeneo madogo ambamo watu hufahamiana kirahisi
kwamba , ni lazima kuongozwa na misingi ya uaminifu na Ukweli . Ukweli unaotoka ndani
ya moyo.
Papa aliwataka wote waliokuwa wamefika katika Ibada hyo, kila mmoja
wao kuitafakari hali ya nafsi yake kama ni safi au chafu , ni kufikiri kilichomo ndani
ya moyo na kuoana kama "Kuna upendo? Au kuna chuki ? Na iwapo kuna tabia ya msamaha
kwa wale wanaotukosea na kutuumiza kimaisha au kuna tabia ya kulipa kisasi . Alikazia
ni muhimu kujiuliza kilichomo ndani kwa sababu ndani ya hutoka yote matenda uovu,
au wema . Na wema huupata uhuru moyo kuliko uovu.
Papa amekiri, ni kweli,
kusamehe na kuwa mtu mwema si rahisi, lakini ni muhimu katika kuyatembea maisha matakatifu
hasa katika kumpokea Bwana,na kuomba aingilie kati maisha yetu. Ni daima kuiomba
neema hii ya kujua nini kinaendelea ndani ya moyo, na daima kufanya uchaguzi sahihi
, uchaguzi wa mzuri. Ni kukumbuka kwamba matendo maovu katika maisha yetu huchafua
roho zetu na kutuweka mbali na Bwana. Tuombe Bwana atusaidie daima, kuwa karibu nae,
Papa alisisitiza. .
Hii ilikuw ani Parokia ya nne kutembelewa na Papa Francisko
tangu kuanza utume wake mwaka jana. Mwishoni mwa Misa, Papa alitoa na shukrani kwa
Paroko Padre Antonio d' Errico wa Parokia ya Mtakatifu Thomas Mtume, ambayo iko
katika eneo lenye hili maarufu la Infernettalenye wakazi wapatao 25,000.