2014-02-17 11:42:57

Wagonjwa msikate tamaa, Kristo yuko karibu nanyi!


Hivi karibuni, Mama Kanisa ameadhimisha Siku ya 22 ya Wagonjwa Duniani kwa kuitaka Jumuiya ya Waamini kujenga na kuimarisha mshikamano wa upendo na wagonjwa.

Wagonjwa nao wakakumbushwa kwamba, wanao mchango mkubwa katika maisha na utume wa Kanisa, kwani wao bado ni sehemu ya Fumbo la Mwili wa Kristo, yaani Kanisa hata katika mahangaiko na magonjwa yao!

Leo Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anawasihi wagonjwa wasikate tamaa hata wanapokabiliana na hali ngumu ya magonjwa yao, bali waendeleee kuwa na matumaini, kwani Yesu Kristo daima yuko karibu nao!







All the contents on this site are copyrighted ©.