Umoja wa Mataifa unaangalia uwezekano wa kuendeleza vikwazo vvya biashara ya silaha
nchini Somalia
Taarifa ya wataalam wa mambo ya ulinzi na usalama kutoka Umoja wa Mataifa inaonesha
kwamba, hali ya ulinzi na usalama bado ni tete nchini Somalia, jambo ambalo limeridhiwa
na Serikali ya Somalia. Kutokana na ukweli huu, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
linangalia uwezekano wa kuendelea kuiwekea vikwazo vya biashara ya silaha Somalia
ilivyowekewa kunako Mwaka 1992 ili kuimarisha ulinzi na usalama.
Wachunguzi
wa mambo wanasema, kuregezwa kwa vikwazo vya silaha nchini Somalia, kwa miaka ya hivi
karibuni, kumekuwa ni chanzo cha machafuko ya hali ya kisiasa na kijamii nchini Somalia.
Wazo la kuendeleza vikwazo vya biashara ya silaha nchini Somalia lilikwisha tolewa
na Mashirika ya Misaada ya Kimataifa pamoja na vyama vya kiraia, kwani biashara ya
silaha ikiruhusiwa nchini Somalia, maisha ya watu wengi yatakuwa hatarini kwani zinaweza
kuangukia mikononi mwa watu vikosi vya waasi na vikundi vya kigaidi!