2014-02-17 15:28:26

Umbeya na porojo za uongo huweza kuua, Papa aonya


Vatican : Jumapili watu wapatao elfu 50 walifurika katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro la Vatican kusali na Papa sala ya Malaika wa Bwana. Kama yalivyo mazoea, kabla ya sala ya hiyo, Papa alitoa hotuba fupi ambayo aliingalisha katika ujumbe kutoka somo la Injili ya Jumapili , akikumbusha kwamba , Upendo wa Bwana hauna kipimo wala mipaka, Mathayo ( 5:17-37 ).

Papa alionya dhidi ya vimaneno maneno , na porojo za uongo na visingizio kwamba huweza kuua. Hinyo , alikumbusha umuhimu wa kuwa wakweli na kukaaq kw amani na jirani zetu. Na aliutaja upendo wa Bwana kuwa ni mkubwa usio kuwa na kipimo wala kuhesabika . .

Papa Francisko katika hotuba yake aliitafakari Injili ya Hotuba ya Mlimani ya Yesu, hotuba ya kwanza kubwa katika mahubiri ya Yesu. Na jinsi Yesu alivyoheshimu sheria za Wayahaudi akiSema ziliwawezesha kuishi katika utimilifu wa amri za Mungu zilizotajwa na Musa . Na kwamba, hili ni hitaji katika utendaji wa haki na ukweli halisi. Papa alilenga zaidi katika amri ya tano” Usiue”

Aliendelea kufundisha kwamba, Yesu pia alikumbusha juu ya amri hii kwamba hata maneno yanaweza kuua! Pale tunaposema mtu mwenye ulimi wa nyoka , ni nini maana yake nini? Ni kwamba maneno yake yana sumu , yanaweza kuua! Na hivyo si tu huyaweka maisha ya wengine katika majaribu, lakini pia huweka sumu ya hasira ya kulipiza kisasi au kuvumisha uzushi dhidi ya wengine.

Papa amesema , sasa basi midomo hii ya uzushi , na porojo za umbeya na chuki, kwa sababu huuua na kuua si sifa ya ubinadamu.Amesema mara ya kwanza, tunaweza kuyafurahia maneno hayo ya uzushi ikionekana kama jambo zuri, kama ilivyo pipi, lakini mwisho huijaza moyo uchungu na sumu. Papa amesisitiza, kila mmoja lazima ajiepushe na tabia hiyo. Papa ametaka uwepo wa mazungumzo na barizi zinazoongoza katika utakatifu.

Ni kuifuta njia ya upendo mtimilifu , upendo usiokuwa na kipimo au kuhesabika uliotangazwa na Yesu. Ni upendo unaokwenda zaidi ya hesabu kwa watu wote. Upendo kwa jirani ni tabia ya msingi iliyohimizwa na Yesu katika kujenga uhusiano na Mungu, na haiwezekani kuwepo mahusiano mazuri na Mungu kama hatutaki kujipatanisha na jirani na kuishi kwa amani na wengine. Katika mwanga wa mafundisho ya Kristo , hivyo , tunaona umuhimu wa kuchunguza na kudhibiti mienendo na matendo yetu, katika misingi ya Sheria za Mungu.

Na kw aajili ya kudumisha tabia nzuri na ukweli haitoshi kuzishikilia sheria , lakini tunahitaji vichocheo vya kina , vinavyoonyesha siri ya kuipata hekima, Hekima ya Mungu , ambayo tunaweza kupokea kwa njia ya Roho Mtakatifu. Na kwa njia ya imani katika Kristo tunaweza kujifunua wenyewe kwa uwezo wa Roho Mtakatifu ambaye daima hutuwezesha kuishi katika upendo wa Mungu.

Katika mwanga wa mafundisho ya haya ya Kristo, kila amri inaonyesha maana yake kamili katika mahitaji ya upendo, wote wakijiwemka pamoja katika kuitii amri kuu : kumpenda Mungu kwa moyo wako wote na upendo jirani kama nafsi yako.

Baada ya sala ya Malaika wa Bwana Papa alitoa salaam zake za upendo wa kibaba kwa mahujaji na wageni waliokuwa wakimsikiliza akiyataja makundi makubwa ya waamini waliotoka Jamhuri ya Czech ambao unaambatana maaskofu wao, waliokuwa wakikamiisha ziara yao ya ad limina visita. Na makundi makubwa ya mahujaji toka Hispania, Vijana wa Kikundi cha Guanelli na kundi la askari wa Italia .








All the contents on this site are copyrighted ©.