2014-02-15 15:33:22

Askofu Ndzando amefariki dunia Jimboni Lisala, DRC


Askofu mstaafu Louis Nganga wa Ndzando wa Jimbo Katoliki Lisala, nchini DRC, amefariki dunia tarehe 13 Februari, 2014 akiwa na umri wa miaka 91. Marehemu Askofu mstaafu Ndzando alizaliwa Jimboni Lisala kunako mwaka 1923. Akapadrishwa tarehe 22 Februari 1953.

Tarehe 18 Aprili 1961 akateuliwa kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki Lisala na kuwekwa wakfu hapo tarehe 9 Julai 1961. Baba Mtakatifu Paulo wa Sita, kunako tarehe 25 Novemba 1964 akamteua kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Lisala, nchini DRC.

Baada ya utume wa kufundisha, kuongoza na kuwatakatifuza Watu wa Mungu Jimbo Katoliki Lisala, tarehe 6 Julai 1997 akang'atuka kutoka madarakani kadiri ya sheria za Kanisa. Ibada ya mazishi yake, imefanyika Jumamosi tarehe 15 Februari 2014 Jimboni Lisala, DRC.







All the contents on this site are copyrighted ©.