2014-02-14 08:08:04

Mikakati ya Kanisa katika kuwahudumia wazee wenye ulemavu!


Taasisi ya Kipapa kuhusu Uhai, itaanza mkutano wake wa Mwaka hapo tarehe 19 Februari hadi tarehe 22 Februari 2014 kwa kuongozwa na kauli mbiu “Uzee na Ulemavu. RealAudioMP3

Baada ya Maadhimisho ya mkutano mkuu wa Taasisi ya Kipapa kuhusu uhai, kama sehemu ya kumbu kumbu ya Maadhimisho ya Miaka 20 tangu ilipoanzishwa na Mwenyeheri Yohane Paulo wa Pili ili kulinda na kutetea Injili ya Uhai, Taasisi itatoa nafasi kwa watu kutoka nje ili kushiriki katika warsha itakayoendeshwa na mabingwa katika sekta ya huduma kwa wazee pamoja na tatizo la ulemavu linaloendelea kukabiliana na vizingiti mbali mbali kutokana na myumbo wa uchumi kimataifa pamoja na sera za Serikali nyingi kutaka kubana matumizi.

Taasisi hii hivi karibuni ilichapisha ajenda za mkutano mkuu uliofanyika kunako Mwaka 2013 kwa kuongozwa na kauli mbiu: “Imani na maisha ya binadamu”. Wajumbe katika warsha hii watajadili pamoja na mambo mengine kuhusu: utamaduni wa ulemavu miongoni mwa wazee, utu na maadili; hati na sera za kimataifa kuhusu huduma kwa wazee wenye ulemavu; takwimu zilizopo, magonjwa kwa wazee, tafiti na dawa zilizopo; huduma kwa wazee katika Jamii, taalimungu kuhusu wazee wagonjwa.

Washiriki wataangalia kuhus: matatizo na changamoto za kimaadili na utatuzi wake; tasaufi na wazee wagonjwa na mwishoni, Kanisa katika kuwahudumia wazee wagonjwa, tema itakayochambuliwa na Askofu mkuu Zymunt Zimowski, Rais wa Baraza la Kipapa la huduma za kichungaji kwa wafanyakazi katika sekta ya afya.








All the contents on this site are copyrighted ©.