2014-02-13 08:42:42

Kumbukumbu ya Miaka 83 tangu kuanzishwa kwa Radio Vatican


Radio Vatican, Mama wa Radio zote duniani, tarehe 12 Februari 2014 imeadhimisha kumbu kumbu ya Miaka 83 tangu ilipoanzishwa. Inajivunia kuwa ni kati ya wadau wakuu wa Shirikisho la Watangazaji Barani Ulaya, EBU ambalo tarehe 13 Februari 2014 linaadhimisha Siku ya Radio Duniani. Kwa namna ya pekee, Jumuiya ya Kimataifa kwa mwaka huu, inajielekeza zaidi katika kuangalia mchango wa wanawake katika medani mbali mbali za maisha.

Watangazaji wanawake kutoka Radio Vatican wamekuwa mstari wa mbele kwa kuwa ni sauti ya wanawake wasiokuwa na sauti kutoka sehemu mbali mbali za dunia. Radio Vatican katika mtandao wake imeandaa programe mbali mbali zinazoonesha mchango wa Radio Vatican katika kuwawezesha wanawake Barani Afrika, Asia na Amerika.

Hizi ni programme zinazoonesha ujasiri wa wanawake katika kukabiliana na changamoto mbali mbali za maisha: katika masuala ya maendeleo endelevu, haki na amani duniani. Ukitaka kufaidi zaidi unaweza kutembelea katika tovuti rasmi ya Radio Vatican kwa anuani ifuatayo: www.radiovaticana.va
Unaweza pia kuwashirikisha jirani zako.







All the contents on this site are copyrighted ©.