2014-02-13 11:45:08

13 Februari 2014 ni Siku ya Radio Duniani


Tarehe 13 Februari ni Siku ya Redio ya Dunia, iliyopitishwa na Mkutano Mkuu wa 36 wa Baraza la UNESCO Novemba 3, 2011, kwa azimio la Bodi Tendaji la 187, kuwa na Siku maalum kwa ajili ya chombo cha Redio, katika kuona umuhimu wake duniani , kama chombo cha kufanikisha uboreshaji ushirikiano ndani kitaifa na kimataifa na katika kuhimiza mitandao mikubwa ya njia za mawasiliano na redio mahalia kukuza uhuru wa kujieleza na usawa wa jenda kupitia mawimbi ya redio .

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kitoa hotuba yake kwa ajili ya adhimisho hili amesema, kwa mwaka huu, wanalega zaidi katika kukuza sauti ya wanawake katika utaganzaji redioni ambao kwa wakati huu ni asilimia 25 tu ya watangazaji wote redioni.......

Shirika la Umoja wa Mataifa la Utamaduni , Elimu na sayansi UNESCO , kama Shirika Mama katika mawasiliano ya Redio, ngazi ya Umoja wa Mataifa, kwenye maadhimisho ya mwaka huu limesema, pamoja na maendeleo makubwa katika mfumo wa digitali, Redio bado inaendela kubakia kuwa njia muhimu ya haraka sana katika mawasiliano ya binadamu mahali popote, na katika wepesi kuelimisha habari juu ya masuala ya kijenda na hasa manufaa ya kuwawezesha wanawake duniani, hata katika maeneo yaliyo sahaulika kimaendeleo, kama vijiji vya ndani mbungani au misituni , ambako hakuna hata nishati ya umeme. na barabara.

Msemaji wa Redio ya Moja wa Mataifa Derrick Mbatha , akiizungumzia siku hii ametaja kati ya Malengo ya UNESCO, ya Siku ya Dunia ya Redio, 2014 kwamba ni Kuhamasisha wamiliki wa vituo vya Redio, wafanyakazi, wanahabari, na serikali kutengeneza sera endelevu katika usawa wa jenda katika mipango mbinu ya Redio.
Pii ni kuondokana na mipango ya kurudia yaleyale badala yake, kuwe na mipango ya utangazji ya redio yenye kukuza mitazamo mbalimbali katika taswira na utendaji .
Tatu, ilenge kujenga uzoefu kwa vijana kupitia mipango ya redio, kwa vijana wote kike na kiume, ili waweze kuwa na moyo wa kutoa habari sahihi na pia wawe na hamu ya kufuatilia vipindi vya redioni, kama njia ya kuwaongezea elimu na ujuzi.

Pia , maadhimisho ya mwaka huu yanalenga kukuza usalama wa waandishi wa habari na watangazaji wanawake , kama alivyoeleza Mirta Lourenzo , Mkuu wa kitengo cha Maendeleo katiak mawasilaino na jamii wa UNESCO. .

UNESCO imetoa mwaliko kwa nchi zote kupanga shughuli za Redio kwa kushirikiana na watangazaji wa kimkoa, kitaifa na kimataifa , mashirka ya kujitegemea , vyombo vya habari mahalia na umma kwa ujumla, hasa katika kufanikisha lengo kuu la mwaka huu kukuza zaidi usawa jenda kupitia mfumo wa habari kwa njia ya rediio, kama njia msingi ya kukuza usawa wa kijenda na uwezeshaji wanawake duniani kote. UNESCO inazidi kusema, bado kuna mengi ya kufanyika , katika kukuza usawa kati ya wanawake na wanaume wanaofanyakazi katika vituo vya Redio.

Na kwamba, Redio bado ni chombo Kikuu katika utoaji wa habari, kuelimisha na kuhamasisha watu mahali popote duniani, katika masuala yanayowahusu kijamii. Na bado ni chombo kinachoweza kununuliwa kwa gharama nafuu.
Hivyo redio ni rafiki wa karibuni sana watu hasa masikini , kwani redio huweza kuriwadha, kuelimisha, kupasha habari na kuwaburudisha pia bila kujali hadhi au lika na hali ingine yoyote ile. Hata katika mabadiliko ya nyakati hizi ambamo teknolijia ya simu za mkononi na tableti, inashika kasi ya kwanza katika upashanaji habari, bado chombo cha redio ni njia kuu ya nyepesi ya kuutaarifu umma mara moja kwa ujumla.

Katika kuiadhimisha Siku hii, Tracey MacClure, kwa niaba ya wanahabari wa kike wa Redio Vatican anasema, mchango wao ni kutoa sauti kwa niaba ya sauti za mamillioni ya wanawake wasioweza kusikika duniani. Wanawake wanaoishi k atika hali mazingira magumu na hatarihi kama maeneo ya vita na ghasia mara nyingi unaosababisha na ubabe wa wanaume na katika maeneo mengine ambako madhulumu dhidi ya wanawake ni maisha ya kila siku.

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu kuhusu ukatili wa kingono katika maeneo ya vita, Zainab Hawa Bangura, amesema kuna haja ya kila mmoja kuhakikisha kuwa wanawake jasiri ambao wanamulika hali ya maisha ya wanawake wanaodhulumiwa katika migogoro, ni lazima wanalindwe.

Akihojiwa na Redio ya Umoja wa Mataifa kuhusu siku ya Redio Duniani, Februari 13, Bi Bangura amesema njia mojawpo ya kuwawezesha wanawake, kupata habari kuhusu haki na masuala wanayopaswa kujua.

Ameongeza kuwa, katika kazi yake, watu wengi ambao wanaathiriwa na uhalifu wa ukatili wa kingono wanaishi vijijini, ambako hawana umeme na wala njia za usafiri, na njia pekee ya kuwafikia ni kupitia redio.

Na kwamba , Redio, siyo tu inawaelimisha, lakini inaongeza uelewa, huwapa fursa na huwaunganisha na huduma na kuwafanya wajue kuwa kile ambacho kimekuwa kikifanyika dhidi yao ni uhalifu, unaopaswa kutolewa taarifa. Ni uhalifu dhidi ya sheria ya kimataifa. Kwa mfano katika DRC, hakuna mitandao ya barabara kati ya Kinshasa na Goma, kwa hiyo njia pekee ya kupata habari za wanawake wanaokumbana na madhulumu ya kubakwa na maaskari dhalimu, ni kupitia redio mahalia ya FM. Hivyo wa hiyo Redio ndicho chombo pekee bora kabisa ambacho kimesaidia katika kukabiliana na tatizo la ukatili wa kingono na tohara haramu kwa wanawake,Redio Umoja wa Mataifa imetaarifu hayo. .







All the contents on this site are copyrighted ©.