Tarehe 10 februari 2014, Vatican na Serikali ya Hungaria zimebadilishana hati za makubaliano
kati ya nchi hizi mbili. Askofu mkuu Alberto Bottari de Castello, Balozi wa Vatican
nchini Hungaria ameongoza ujumbe wa Vatican katika halfa hii. Kwa upande wa Serikali
ya Hungaria, Dr. Zoltan Balog, Waziri wa rasilimali watu nchini Hungaria ameongoza
ujumbe wa nchi yake.
Hati hizi zimefanya marekebisho ya msingi katika makubaliano
yaliyokuwa yametiwa sahihi kati ya pande hizi mbili kunako tarehe 20 Juni 1997 kuhusu
ruzuku ya fedha kwa huduma za kijamii zinaztolewa na Kanisa nchini Hungaria na mambo
mengine yanayohusu urithi wa Kanisa nchini Hungaria, mkataba uliokuwa umetiwa sahihi
tarehe 21 Oktoba 2013. baada ya kubadilishana hati za mkataba kadiri ya Ibara 7 ยง
kifungu cha 2 mkataba huu umeanza kutekelezwa rasmi.