2014-02-11 13:39:45

Wagonjwa mkumbatieni Kristo Msulubiwa, yuko karibu nanyi daima!


Mama Kanisa tarehe 11 Februari 2014 anaadhimisha Siku ya 22 ya Wagonjwa Duniani inayoongozwa na kauli mbiu "Imani na upendo: imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu. 1 Yoh. 3:16. Wagonjwa wanakumbushwa kwamba, wao ni sehemu muhimu sana katika Fumbo la Mwili wa Kristo yaani Kanisa. Wanabeba pamoja na Kristo mahangaiko yao ya ndani!

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii, anapenda kuchukua fursa hii kuwatakia wagonjwa na wote wanaoteseka kheri na baraka katika Maadhimisho ya Siku ya Wagonjwa Duniani. Watambue kwamba, Yesu Kristo Msulubiwa yuko karibu nao: changamoto ya kumkumbatia kwa nguvu zote.







All the contents on this site are copyrighted ©.