2014-02-11 10:24:26

Tumwombee Papa mstaafu Benedikto XVI


Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii, anawaalika kwa namna ya pekee tarehe 11 Februari 2014 kuungana naye kusali kwa ajili ya kumwombea Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto wa kumi na sita; kiongozi aliyeonesha ujasiri na unyenyekevu.

Itakumbukwa kwamba, umepita mwaka mmoja, tangu Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI alipong'atuka kutoka madarakani kutokana na uzee ili kutoa nafasi kwa Kiongozi mwingine wa Kanisa aweze kuwaongoza Watu wa Mungu kwa kasi na moyo mkuu, kama anavyofanya kwa sasa Papa Francisko.







All the contents on this site are copyrighted ©.