2014-02-11 13:39:07

Mheshimiwa Padre John Joale Tlhomola ateuliwa kuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Mohale's Hoek, Lesotho


Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi lililowashirikishwa kwake na Askofu Sebastain Khoarai wa Jimbo Katoliki la Mohale's Hoek, nchini Lesotho kadiri ya Sheria za Kanisa namba 401 Ibara ya1. Baba Mtakatifu amemteua Mheshimiwa Padre John Joale Tlhomola; Mkuu wa Shirika la Mapadre Watumishi wa Kristo, Jimbo kuu la Pretoria, Afrika ya Kusini kuwa Askofu Mpya wa Jimbo Katoliki la Mohale's Hoek, nchini Lesotho.

Askofu mteule John Joale Tlhomola alizaliwa kunako tarehe 12 Machi 1966 Jimbo kuu la Maseru. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapadrishwa tarehe 28 Machi 1998. Tangu wakati huo ametekeleza utume wake wa Kipadre katika sehemu mbali mbali hadi mwaka 2011 alipochaguliwa kuwa ni Mkuu wa Shirika la Mapadre Watumishi wa Kristo, Jimbo kuu la Pretoria, Afrika ya Kusini.







All the contents on this site are copyrighted ©.