Waombeeni Mapadre wenu waaminifu wanaojisadaka kwa ajili ya ndugu zao katika Kristo
Kuna kundi kubwa la Mapadre wema na watakatifu wanaoendelea kujitosa bila ya kujibakiza
kwa ajili ya kuwahudumia watu wa Mungu sehemu mbali mbali za dunia kiroho na kimwili.
Hawa ni wahudumu wa Neno la Mungu, Sakramenti za Kanisa na Matendo ya huruma. Ni watu
wanaojisadaka hata kwa gharama ya maisha yao wenyewe!
Baba Mtakatifu Francisko
katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii, anawaalika waamini na watu
wote wenye mapenzi mema kusali na kuwaombea Mapadre wema na watakatifu wanaojisadaka
kwa ajili ya ndugu zao katika Kristo kwa ukarimu, unyenyekevu bila hata ya kutafuta
makuu!