2014-02-07 07:32:30

Simameni kidete kupinga biashara haramu ya binadamu!


Tarehe 8 Februari, kila mwaka, Mama Kanisa anaadhimisha Kumbu kumbu ya Mtakatifu Josephina Bakhita, Mtawa kutoka Sudan aliyekumbukana na madhulumu na nyanyaso kiasi cha kuuzwa utumwani. Akaonja huruma na upendo wa Mungu na kubahatika kukombolewa kutoka utumwani. RealAudioMP3
Katika hija ya maisha yake, akabahatika kuwa Mtawa wa Shirika la Mabinti wa Upendo wa Mtakatifu Madgalena wa Canossa.
Baraza la Maaskofu Katoliki Marekani, linatumia tarehe 8 Februari kuhamasisha watu kuhusu madhara ya biashara ya binadamu inayoendelea kushika kasi ya ajabu duniani kutokana na ubinafsi pamoja na uchu wa mali na utajiri wa haraka haraka. Waamini na watu wenye mapenzi mema, wanahamasishwa kuangalia madhara yanayotokana na biashara haramu ya binadamu kwani vitendo hivi ni kinyume cha ubinadamu!
Waamini na wananchi wenye mapenzi mema wanapaswa kusimama kidete kulinda na kutetea utu na heshima ya binadamu, aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu na kukombolewa kwa Damu Azizi ya Yesu Kristo.








All the contents on this site are copyrighted ©.