2014-02-07 07:48:43

Balozi Bassim awasilisha hati za utambulisho kwa Papa Francisko


Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 6 Februari 2014 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Bi Wafaa Ashraf Moharram Bassim, Balozi Mpya wa Misri mjini Vatican. Bi Bassim alizaliwa kunako tarehe 21 Mei 1955 huko Heliopolis, ameolewa na ana watoto watatu.

Balozi Bassim ana shahada ya uzamivu katika masuala ya kiuchumi. Tangu mwaka 1978 amekuwa katika masuala ya kidplomasia kwenye Ubalozi wa Misri nchini Italia; Mwakilishi wa Misri kwenye Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyoko mjini Geneva. Balozi, Naibu Waziri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa. Uongozi wa Vatican unamtakia kheri na baraka Balozi Wafaa Ashraf Moharram Bassim katika dhamana na utume wake mjini Vatican.







All the contents on this site are copyrighted ©.