2014-02-06 09:30:38

Watu 500 walipoteza maisha kutokana na vita ya kikabila nchini Kenya


Taarifa ya Umoja wa Mataifa inaonesha kwamba, katika kipindi cha Mwaka 2013 watu elfu tano walipoteza maisha katika mapambano ya kikabila; kinzani kati ya wakulima na wafugaji pamoja na uhasama wa kisiasa nchini Kenya. Kuna idadi kubwa ya wananchi waliojeruhiwa na zaidi ya watu laki tano walilazimika kuyakimbia makazi yao.

Taarifa hii imetolewa mapema juma hili na Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu misaada ya kibinadamu. Idadi kubwa ya watu waliofariki dunia ni wale waliokumbwa katika mapigano yaliyotokea Mwezi Desemba sehemu za Moyale, Mandera na kwenye Bonde la Mto Tana.







All the contents on this site are copyrighted ©.