2014-02-06 11:34:56

Siku ya Kimataifa ya kupambana na tabia ya Ukeketaji!


Jumuiya ya Kimataifa kila Mwaka tarehe 6 Februari inaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Tabia ya Ukeketaji. Shirika la kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF linasema kwamba, kuna zaidi ya watoto, wasichana na wanawake millioni 120 ambao wamekumbana na ukatili wa kukeketwa kutoka sehemu mbali mbali za dunia.

Katika kipindi cha miaka kumi ijayo, watoto zaidi ya millioni 30 wanahofiwa kwamba, wanaweza kukeketwa. Nchi zinazoongoza Barani Afrika ni Somalia, Guinea, Djibuti na Misri. Mila hizi ambazo zimepitwa na wakati zinaendelea kutekelezwa nchini Chad, Gambia, Mali, Senegal, Sudan na Yemen.

Ikumbukwe kwamba, ukeketaji ni uvunjwaji wa haki msingi za wanawake katika masuala ya afya, changamoto kwa wadau mbali mbali kusimama kidete kupinga mila na desturi hizi ambazo zinaendelea kuhatarisha maisha ya watoto, wasichana na wanawake wengi duniani.







All the contents on this site are copyrighted ©.