Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu amefanya mabadiliko ya baadhi ya makamanda
wa mikoa, wakuu wa upelelezi wa mikoa, wakuu wa usalama barabarani wa mikoa pamoja
na watendaji wengine wa vikosi na vitengo mbalimbali ndani ya Jeshi la Polisi.
Miongoni
mwa makamanda wa mikoa waliofanyiwa mabadiliko ni pamoja na aliyekuwa kamanda wa Mkoa
wa Ruvuma Kamishna msaidizi mwandamizi (SACP) Deusdedit Nsimeki anayekwenda kuwa
kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara, Aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara kamishna
msaidizi (ACP) Akili Mpwapwa anakwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma.
Wengine
ni aliyekuwa Afisa Mnadhimu mkoa wa Lindi Kamishna msaidizi (ACP) Renatha Mzinga anakuwa
Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi, aliyekuwa afisa Mnadhimu Mkoa wa Dodoma Kamishna
msaidizi wa Polisi (ACP) Suzan Kaganda amehamishwa kwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa
wa Tabora na aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora kamishna msaidizi (ACP) Peter
Ouma amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi.
Zaidi ya hao wengine waliyohamishwa
ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa upelelezi Mkoa wa Mtwara Kamishna msaidizi wa Polisi
(ACP) Eliyakimu Masenga anakwenda kuwa Mkuu wa upelelezi kikosi cha Tazara, aliyekuwa
mkuu wa upelelezi Mkoa wa Tabora Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) David Mnyambuga
anakwenda kuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Ilala, na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa
wa Ilala, Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Juma Bwire, anakwenda kuwa Afisa Mnadhimu
Mkoa wa Tabora .
Aidha, aliyekuwa afisa Mnadhimu mkoa wa Tabora Mrakibu Mwandamizi
wa Polisi (SSP) John Kauga anakuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Tabora, aliyekuwa Mkuu
wa Polisi wa wilaya ya Rombo (SSP) Mrakibu mwandamizi Ralph Meela anakwenda kuwa mkuu
wa upelelezi mkoa wa Mtwara na aliyekuwa Mkuu wa upelelezi wa kikosi cha Tazara Mrakibu
wa Polisi (SP) Isack Msengi anakwenda kuwa Kaimu mkuu wa upelelezi mkoa wa Pwani.
Kwa
upande wa wakuu wa Polisi wa mikoa wa Usalama Barabarani ni pamoja na aliyekuwa Mkuu
wa Trafiki Mkoa wa Kinondoni, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Ibrahim Mwamakula
ambaye amehamishiwa Trafiki Kanda Maalum Dar es Salaam, aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa
wilaya ya Mtwara, Mrakibu wa Polisi (SP) Awadh Haji anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki
Mkoa wa Kinondoni, na Mrakibu wa Polisi (SP) Ezekiel Kiko Mgeni aliyekuwa ofisi ya
RPC Temeke, anakuwa Mkuu wa Trafiki mkoa wa Temeke.
Wengine ni aliyekuwa Mkuu
wa Trafiki Mkoa wa Lindi Mrakibu wa Polisi (SP) James Kiteleki anakwenda kuwa Mkuu
wa Trafiki Mkoa wa Njombe, aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Ilala, Mrakibu wa Polisi
(SP) Meloe Buzema anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Lindi, aliyekuwa Kaimu Mkuu
wa Trafiki Mkoa wa Temeke Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Prackson Kibogoyo anakwenda
kuwa Mkuu wa Operesheni Mkoa wa Pwani, na aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Njombe,
Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Chacha Nsaho Maro anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki
Mkoa wa Ilala.
Mabadiliko hayo ni ya kawaida kwa mujibu wa kanuni,
taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi katika kuhakikisha kwamba wananchi wanaendelea
kupata huduma bora ya usalama.