2014-02-06 14:41:14

Injili inawachangamotisha waamini kujitosa kwa ajili ya jirani zao!


Ni tabia ya binadamu kujipenda na kujitafuta mwenyewe; kuponda mali na kusahau kwamba, kuna maisha baada ya kifo. Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anasema, kwamba, ulimwengu na mazuri yake, yanawafanya watu kujitafuta wenyewe; kuwa na mambo mengi pamoja na kufurahia maisha!

Baba Mtakatifu Francisko anasema, Injili inawaalika na kuwachangamotisha waamini kujitoa katika ubinafsi wao na kuwaendea jirani zao, ili kushirikisha na kuwaonjesa maskini na wote wanaosukumizwa pembezoni yale waliyokirimiwa na Mwenyezi Mungu katika upendo wake.







All the contents on this site are copyrighted ©.