Mbinu mkakati wa kupambana na baa la njaa Ukanda wa Sahel
Shirika la Misaada ya Maendeleo la Watu wa Marekani, USAID katika kipindi cha miaka
miwili, litachangia kiasi cha dolla za kimarekani millioni 130 kama sehemu ya mchakato
wa kusaidia juhudi za Jumuiya ya Kimataifa kupambana na baa la njaa linalotokana na
ukame wa muda mrefu kwenye Ukanda wa Sahel unaozijumuisha nchi za: Burkina Faso, Cameroon,
Chad, Gambia, Mali, Mauritania, Niger, Nigeria pamoja na Senegal. Mchango huu utakuwa
ni wa kipindi cha miaka mitano ili kushiriki kikamilifu katika maboresho ya maisha
ya wananchi vijijini.
Kuna watu zaidi ya millioni ishirini wanaokabiliwa na
baa la njaa Ukanda wa Sahel. Mtu mmoja kati ya kundi la watu nane ndiye mwenye uhakika
wa usalama wa chakula kwenye nchi za Sahel. Serikali ya Marekani inapenda kuchangia
katika mchakato wa maendeleo endelevu katika eneo la Sahel ambalo kwa sasa linakabiliana
na majanga makuba kama vile: umaskini, ukosefu wa uhakika wa usalama wa chakula; ukame
wa muda mrefu, vita pamoja na mashambulizi ya kigaidi.