Askofu mkuu Santo Gangemi ateuliwa kuwa Balozi Mpya wa Vatican nchini Mali
Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Santo Gangemi, kuwa Balozi Mpya wa Vatican
nchini Mali na ataendelea pia kuwa ni Balozi wa Vatican nchini Guinea. Hiki ni kielelezo
cha mshikamano wa dhati kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko kwa watu wanaoendelea
kuteseka kutokana na majanga mbali mbali ya maisha Barani Afrika.
Baba Mtakatifu
anaendelea kuhimiza majadiliano katika ukweli, uwazi na udugu kama njia ya kupambana
na changamoto mbali mbali zinazoendelea kujitokeza katika maisha ya watu sehemu mbali
mbali za dunia, hususan migogoro ya kivita na kinzani za kijamii kama ilivyo nchini
Mali.