2014-02-04 09:58:16

Urithi wa Mzee Madiba ni kiasi cha dolla za Kimarekani millioni 4.1


Hayati Mzee Nelson Mandela ameacha urithi wa dolla millioni 4.1 zitakazogawanywa kwa mke wake Graca Machel ambaye ana haki ya kupata nusu ya urithi wote; sehemu ya mali itagawanywa kwa wanafamilia, wafanyakazi, shule pamoja na Chama cha tawala cha ANC. Hayo yamo kwenye wosia wa Mzee Mandela uliosomwa mahakamani, Jumatatu tarehe 3 Februari 2014.

Katika wosia huu, Winnie Madikizela- Mandela hakutajwa kati ya watu wanaopaswa kufaidi na urithi ulioachwa na Mzee Madiba aliyefariki dunia tarehe 5 Desemba 2013 na kuzikwa siku 10 baaye kwenye Kijiji chake cha asili huko Qunu, baada ya wakuu wa Jumuiya ya Kimataifa kutoa heshima zao za mwisho kwa Mzee Madiba ambaye baada ya kushinda kinyang'anyiro cha Urais kunako mwaka 1994 alijikita katika siasa ya ukweli na upatanisho, jambo ambalo lilimejengea sifa na heshima kubwa ndani na nje ya Bara la Afrika.







All the contents on this site are copyrighted ©.