Mshikamano wa kidugu na watu waliokumbwa na mafuriko nchini Italia!
Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya kuadhimisha Siku kuu ya kutolewa Bwana Hekaluni
sanjari na Maadhimisho ya Siku ya 18 ya Watawa Duniani, Jumapili tarehe 2 Januari
2014, wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana, aliyaelekeza mawazo yake kwa wananchi wengi
wa Italia ambao kwa wakati huu wamekumbwa na mafuriko ambayo tayari yamekwisha sababisha
maafa makubwa kwa watu na mali zao!
Baba Mtakatifu anawaalika waamini na watu
wenye mapenzi mema, kuonesha moyo wa upendo na mshikamano kwa watu walioathirika kwa
mafuriko haya. Kwa upande wake, ataendelea kuwa karibu nao kwa njia ya sala na sadaka
yake.