Mshikamano wa upendo na kidugu kwa wananchi wa Ufilippini!
Askofu mkuu Joseph Kurtz, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Marekani, kuanzia tarehe
2 hadi tarehe 7 Februari 2014 pamoja na ujumbe wake, watakuwa nchini Ufilippini, ili
kutembelea maeneo yaliyoathirika vibaya kutokana na tufani iliyoikumbuka Ufilippini
hapo tarehe 8 Novemba 2013 na hivyo kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao.
Ziara
hii ya upendo na mshikamano wa kidugu imeandaliwa na Shirika la Misaada la Kanisa
Katoliki Marekani, ambalo limepokea kiasi cha dolla za Kimarekani millioni 50 kwa
ajili ya kuwasaidia wananchi wa Ufilippini waliokumbwa na tufani hii. Wakiwa nchini
Ufilippini watapata nafasi ya kuzungumza na kutembelea Makanisa yaliyoathirika zaidi.
Watakutana na kuzungumza na viongozi wa Kanisa nchini Ufilippini.
Changamoto
ya kuwasaidia wananchi wa Ufilippini baada ya kukumbwa na maafa ilitolewa na Kardinali
Timothy Dolan aliyekuwa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Marekani, wazo ambalo
lilifanyiwa kazi na matunda yake yanaonekana kwa sasa. Ni mchango kutoka kwa waamini
na watu wenye mapenzi mema nchini Marekani.