Vatican na Malta watiliana sahihi mkataba kuhusu masuala ya ndoa!
Serikali ya Malta na Vatican, Jumatatu tarehe 27 Januari 2014, zimetiliana sahihi
nyongeza katika mkataba uliokuwa umetiwa sahihi na pande hizi mbili kunako tarehe
3 Februari 1993 kwa kutambua kisheria ndoa zinazofungwa ndani ya Kanisa na Maamuzi
ya Mahakama za Kanisa kuhusu ndoa.
Askofu mkuu Aldo Cavalli, Balozi wa Vatican
nchini Malta ameuwakilisha ujumbe wa Vatican katika tukio hili na serikali ya Malta
imewakilishwa na Bwana Owen Bonnici, Katibu wa Bunge katika masuala ya haki. Protokali
hii ina Ibara kuu nne zinazofanya mabadiliko katika Mkataba uliotiwa sahihi kunako
Mwaka 1993.