2014-01-29 09:34:33

Watu 26 wafariki dunia baada ya Kanisa kushambuliwa nchini Nigeria


Kikundi cha Boko Haram, jumapili iliyopita, tarehe 26 Januari 2014 kimefanya shambulizi katika Kanisa Katoliki, Kaskazini mwa Nigeria na kusababisha vifo vya watu 26. Boko Haram pia ilifanya mashambulizi kwenye baadhi ya nyumba zilizoko karibu na Kanisa.

Viongozi wa Kanisa na Serikali wamekiri kutokea kwa shambulio hili linaloendelea kujenga hofu na wasi wasi miongoni mwa wananchi wa Nigeria, wanaopaswa kushikamana katika umoja na udugu na kutokubali kutumiwa na baadhi ya watu wanaotaka kujinufaisha wenyewe kutokana na migogoro ya kidini.

Itakumbukwa kwamba, kunako tarehe 26 Januari 2014 Kikundi cha Boko Haram kilivamia Vijiji vya Kauwuri na Wala na kusababisha vifo vya watu 54.







All the contents on this site are copyrighted ©.