2014-01-25 16:39:13

Wanawake warithishaji wa Imani kifamilia.


Baba Mtakatifu Francisko akiwahutubia washiriki wa Kongamano la Wanawake la Kitaifa lililoandaliwa na Kituo cha Wanawake cha Italia, alionyesha hamu yake kuwa na ulimwengu wa kazi, na mazingira ya umma yenye kuona umuhimu wa mchango wa kipekee wa wanawake katika mahusiano ya kifamilia ambayo kwa sisi Wakristu , si tu kama utendaji binafsi lakini kama ufunguo wa Kanisa la nyumbani, ambamo mna afya na ustawi wa Kanisa na jamii yenyewe.

Uwepo wa mwanamke katika nyumba huthibitisha umuhimu wa asili yao ya milele katika kurithisha kizazi kipya misingi ya kimaadili na maambukizi ya imani yenyewe. Wawakilishi wa Taasisi hii ya wanawake Italia, walikutana na Papa siku ya Jumamosi mjini Vatican.

Papa alieleza hilo baada ya kutoa shukurani zake za dhati kwa washiriki wa Kongamano, kwa uwepo wa kituo hiki , kinachotimiza karibia miaka sabini tangu kuanzishwa kama uwanja wa elimu na maendeleo ya binadamu na utoaji wa ushuhuda kuhusu jukumu la wanawake katika jamii na kanisa . Na alikiri uwepo wa mabadiliko katika kipindi cha miongo kadhaa iliyopita, mabadiliko ya kitamaduni na kijamii, pamoja na utambulisho na jukumu la wanawake katika familia, kijamii na kikanisa, ushiriki na uwajibikaji wanawake kwa ujumla kwamba umeongezeka.

Mchakato huu wa mabadiliko unaoonekana kuwa muhimu, pia unatambuliwa na na mafundisho ya Mapapa., kam ailivyotajwa kwa namna ya kipekee,katika waraka wa Kitume wa Papa Yohane Paulo 11 wa mwaka 1988, chini ya Jina :Hadhi na wito wa Mwanamke, Mulieris dignitatem, hati iliyoonyesha utambuzi sambamba na mafundisho ya Mtaguso wa Pili , juu ya nguvu ya maadili ya mwanamke , na nguvu yake ya kiroho ( . cf. n 30), na pia kama alivyooleza katika Ujumbe kwa Siku ya Amani Duniani wa 1995, ulioongozwa na mada "Wanawake : Walimu wa amani."

Papa Francisko pia , ametaja na kukiri uwepo wa mchango muhimu wa wanawake katika jamii, na hasa unyeti wa vipaji vya uelewa kwa wengine kama walio wanyonge na wasiojiweza . Na kwamba yeye mwenyewe yuko radhi kuona wanawake wengi wanashiriki katika baadhi ya majukumu ya Kichungaji, yenye kusindikiza na kuandamana na watu , familia na vikundi , katika tafakari za kiteolojia, na anatumaini kwamba, nafasi za kufanya hivyo, zitaongezeka katika uwepo wa kina zaidi wa wanawake ndani ya Kanisa kama ilivyoelezwa katika Barua ya kitume ya Furaha ya Injili “ Evangelii gaudium” , 103).

Papa aliendelea kuonyesha matumaini yake kwamba mwanya huu mpya na majukumu yaliyowekwa wazi kwa wanawake yutaweza kupanua uwepo na shughuli nyingi kwa wanawake, ndani ya ya Kanisa na katika sekta za kiraia na taaluma, bila ya kusahau jukumu la wanawake katika familia. Sifa za unyeti wake wa kipekee katika utu na huruma ,ni utajiri mkubwa wa akili ya mwanamke , inayowakilisha sio tu nguvu ya kweli kwa maisha ya familia, na kwa ajili ya uwepo wa hewa ya utulivu na amani , lakini pia kama hali halisi katika wito wa ubinadamu unavyotakiwa kuwa.

Papa alimalizia hotuba yake kwa kumshikuru Mungu , kwa mwanga wa Neno lake , linalolishwa na neema za Sakramenti , mwanamke Mkristo siku zote, tena na tena hujaribu kutoa jibu katika wito wa Bwana, katika hali halisi ya hali yake. Ni hali ambayo daima hudumisha uwepo wa Kimama wa Mama Maria. Yeye , ambaye alimlinda Mwana wake wa kimungu , aliyefanya muujiza wake wa kwanza katika harusi ya Kana , ambaye alikuwepo pale Kalvari na wakati wa kushuka kwa Roho mtakatifu (Pentekoste), kuonyesha njia ya kwenda, ili kuimarisha maana na nafasi ya wanawake katika jamii kikamilifu na uaminifu wa wao kwa Bwana Yesu Kristo na katika lengo la utume wao duniani .









All the contents on this site are copyrighted ©.