2014-01-24 15:08:03

Rais François Hollande wa Ufaransa akutana na Papa Francisko



Rais François Hollande , wa Jamhuri ya Ufaransa , Ijumaa hii majira ya saa nne na nusu za asubuhi , alifanya ziara fupi Vatican ambako alikutana na Papa Francisko na kuwa na mazungumzo katika hali ya faragha. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa viongozi hao kukutana. Na baada ya hapo Rais Hollande alikutana na Katibu Mkuu wa Vatican , Kardinali Mteule Pietro Parolin.
Mara ya mwisho Rais wa Jamhuri ya Ufaransa, akiwa bado Rais Nicolas Sarkozy, alimtembelea Papa Mstaafu Benedekto Xv1, Octoba 2010, na ziara ya leo imekuwa ni ya nane kwa Rais wa Ufaranza kutembelea Vatican.
Habari zinasema, mazoea ya Marais wa Jamhuri ya Ufaransa kupata muda wa kumtembelea Papa , ni ya tangu wakati wa Rais Georges Pompidou , 1958.
Rais Hollande aliteuliwa kuwa Katibu wa chama cha kishoshalisiti mwaka 1994. Wakati wa Waziri Mkuu Lionel Jospin, Hollande aliteuliwa msemaji wa serikali , kwa kuzingatia uhodari wake katika masuala ya kisiasa na kati ya viongozi wa ujamaa. Na Oktoba 16, 2011 , Hollande alipata kura nyingi za kuwa mpinzani wa rais anayemaliza muda wake Nicolas Sarkozy. Na alichaguliwa kuwa Rais wa Ufaransa , tarehe 16 May 2012 ,kwa kumshinda Sarkozy kwa asilimia 51.6 ya kura zote. Sarkozy alipata asimilia 48.4 ya kura zote.
Pamoja na kutembelea Vatican , Rais Hollande pia analtembelea Serikali ya Italia.








All the contents on this site are copyrighted ©.