2014-01-24 09:52:41

Mzizi wa fitina ya mgogoro wa Urais wakatwa kwa Madagascar kupata Rais mpya!


Rais mteule Henry Rajaonarimampianina wa Madagascar anaapishwa rasmi kuwa Rais wa Madagascar tarehe 25 Januari, 2014 baada ya Mahakama Maalum ya Uchaguzi nchini Madagascar kumtangaza Bwana Rajaonarimampianina kuwa mshindi wa uchaguzi wa Urais tarehe 17 Januari, 2014.

Duru ya kwanza ya uchaguzi huo ilifanyika tarehe 31 Julai, 2013, ambapo hakupatikana mshindi. Katika duru ya pili iliyofanyika tarehe 20 Desemba, 2013, Mahakama Maalum ya Uchaguzi ilitangaza kuwa Bwana Rajaonarimampianina alipata asilimia 53.49 ya kura zote zilizopigwa huku mpinzani wake Bw. Jean Louis Robinson akipata asilimia 46.51.

Itakumbukwa kwamba, Kwa kushirikiana na wanachama wengine wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Tanzania, ambayo ilikuwa mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC kwa mwaka mmoja ulioishia Agosti, 2013, ilitoa mchango mkubwa kuhakikisha Madagascar inaendesha uchaguzi wake katika hali ya amani na utulivu na kwa kuzingatia misingi ya demokrasia, ili kumaliza mgogoro wa kisiasa ulioibuka mwaka 2008 baada ya Bwana Andry Rajoelina kuingia madarakani kwa kusaidiwa na Jeshi.








All the contents on this site are copyrighted ©.